Shaykh Fawzaan - Jumu'ah Mubaarakah Haijathibiti

Hukmu Ya Kupongezana “Jumu’ah Mubaarakah”
 
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
 

 

 

Wanachuoni wakubwa wa Ummah huu wote wamehukumu kuwa haipasi kuamkiana” “Jumu’ah Mubaarakah”. Miongoni mwao ni ‘Allaamah Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) katika fatwa yake hapa chini.

 

 
SWALI:   
 
Nini hukmu ya kuandikiana na kusema Muislamu kwa Muislamu mwenzake kila siku ya Ijumaa “Jumu’ah Mubaarakah” na hutuma katika simu au kumbi za mawasiliano?

 

 
JIBU:  
 

 

Jambo hili halina asili  kwa hiyo ni  BID’AH! Wala haijuzu kupongezana kila Ijumaa. Hili halikupatika dalili yoyote, wala si katika ‘amali za Salaf. Basi ni jambo la kuzushwa. Na siku hizi wazushi wanatumia vibaya simu za mikono na mitandao kutaja hayo na wanaitumia kusambaza bid’ah kwa njia hizi.

 

 
 
 
 
Share