Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad - Sunnah Ni Kujibu Nini Pindi Unapoambiwa 'Fulani Anakusalimia'?

 
Sunnah Ni Kujibu Nini Pindi Unapoambiwa 'Fulani Anakusalimia'?
 
Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad
 

 

 
Aliulizwa Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad (Hafidhwahu Allaah):
 
"Katika Miji yetu kuna ada hii: 'Inaposemwa, 'Fulani anakusalimia, anayesalimiwa hujibu kwa kusema: 'Allaah Akusallim (Akupe amani) wewe na yeye. (Allaahu yusalimuka wa yusalimuhu)"
 
Akajibu (Hafidhwahu Allaah):
 
"Hii hailingani na Sunnah, bali (mtu anapoletewa salaam kutoka kwa mtu wa mbali, anatakiwa) aseme:
"'Alayka wa 'Alayhis Salaam"  (Amani iwe juu yako na juu yake).
 
Japo (kusema), 'Allaah Akusalim wewe na Amsalim yeye' ni du'aa kumuombea yeye usalama na afya, lakini (kujibu), ''Alayka wa 'Alayhis Salaam' ndio Sunnah. Na mtu anatakiwa aje na nyiradi zilizo bora (zilizothibiti).
 
 
[Sharh Sunan Abiy Daawuwd 46/593]
 
 
Share