Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Sha'baan: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alikuwa Akifunga Zaidi Sha'baan

Miongoni Mwa Fadhila Za Mwezi Wa Sha’baan:

  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alikuwa Akifunga Zaidi Kuliko Miezi Mingine

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

www.alhidaaya.com

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: 

“Ama kuhusu Sha’baan, Naam! Ni mwezi makhsusi kuliko mingineyo kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikithirisha kufunga Swiyaam, bali alikuwa akifunga Swiyaam mwezi wote isipokuwa kidogo tu. Kwa hiyo inapasa kukithirisha Swiyaam katika Sha’baan.”

[Liqaa Al-Baab Al-Maftuwh, 174]