Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kuvaa Kope Za Bandia

 

Kuvaa Kope Za Bandia    

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya mwanamke kuvaa kope za bandia?

 

 

JIBU:

 

Kope za bandia haziruhusiwi kwa sababu (hukmu yake) inafanana na hukmu kuunga nywele  na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani anayeunga nywele na anayeungwa.

 

Na hizo kope zikiwa kama ninavyodhania siku hizi zinatengenezwa kutokana na nyuzi nyeusi kama nywele na kuvaliwa kama kope kuzifanya zionenakane nyingi na kufanya macho yaonekane mazuri, basi hivi ni kama kuunga nywele jambo ambalo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani anayeunga na anayeungwa...

 

 

[Imaam Ibn ‘Uthyamiyn, Fataawa Nuwr ‘Alad-Darb (5626) (11/82)]

 

Share