Kumlipa Ubaya Aliyekutendea Maovu

SWALI:

Kumrudishia mtu mabaya aliyokufanyia unalipwa dhambi? Sina zaidi ni mwana funzi wenu.             

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Si vizuri kwa mtu kumrudishia mabaya mwenziwe bali Muislamu anatakiwa asamehe na kwa hilo linampatia sifa nyingi ambazo hazifikiwi na wengine. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuachia mifano chungu nzima kwa kuwasamehe wapinzani wake pamoja na kuwa walimtesa sana. Na Allaah Anasema:

“Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa” (41: 34 – 35).

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

Share