Kaimati Za Shira Aina Mbali Mbali Caramel, Maziwa Mazito, Asali, Tende

Kaimati Za Shira Aina Mbali Mbali Caramel, Maziwa Mazito, Asali, Tende

Vipimo

Unga - 2 mugs

Hamira - 2 vijiko vya chai mfuto

Yai - 1

Mtindi (yoghurt) - 1 kijiko cha supu

Samli - 2 kijiko vya chakula

Maji - 1 ½ Mug takriban

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Changanya vitu vyote pamoja vizuri upige pige, usiwe mwepesi sana.
  2. Acha uumuke, kisha weka mafuta ya moto uteke vidonge donge kama kawaida ya kaimati.
  3. Kaanga mpaka zigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
  4. Epua chuja mafuta kisha weka katika sahani yenye tissue ya jikoni zizidi kuchuja mafuta.
  5. Gawa katika vyombo vya kupakulia kama bakuli, kisha mwagia shira za aina mbali mbali kama caramel, maziwa mazito (condensed milk), asali, shira ya tende au shira ya kawaida.
  6. Nyunyizia ufuta ukipenda.

Bonyeza upate aina za caramel

 

Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share