Crapes Za Maziwa Kwa Asali

Crapes Za Maziwa Kwa Asali
 
Vipimo

Unga wa ngano - 1 Kikombe

Sukari - 2 Vijiko vya supu

Baking powder - 1 Kijiko cha supu

Chumvi - 1/2  Kijiko cha chai

Mayai - 2

Maziwa - 2 Vikombe

Ngano yakupikika haraka(oats) - 1 Kikombe

Siagi (iliyoyayushwa),au mafuta - 2 Vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka unga, sukari, baking powder na chumvi katika bakuli.
  2. Kwenye bakuli jengine, piga mayai kidogo changanya maziwa, ngano na siagi na iache ikae dakika mbili.
  3. Kisha changanya pamoja na mchanganyiko wa unga.
  4. Weka chuma kisichoganda (non stick) kipate moto.
  5. Paka mafuta kidogo kisha tumia kijiko cha kupakulia tia mchanganyiko iwe duara (kama vibibi).
  6. Itakapoanza kufanya mapovu juu, geuza upande wa pili hadi iive.
  7. Endelea hivyo hivyo mpaka umalize unga wote.
  8. Panga kwenye sahani na tayari kuliwa na asali au shira ya sukari pekee au shira ya matunda kama maple syrup.

Kidokezo

Unaweza kutumia chuma kikubwa kufanya viduara 3 au 4 kwa mara moja

 

Share