Al-Lajnah Ad-Daaimah: Pokemon Ni Mchezo Haraam

 

‘Pokemon’ Ni Mchezo Haraam

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

Alhidaaya.com

 

 

Mufti wa Saudi Arabia, Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Aal Ash-Shaykh (Hafidhwahu Allaah) amesema:

“Waislamu wote wajihadhari na mchezo huu na kuwazuia watoto wao kuucheza.”

Katika Fatwa hiyo ya Kamati Ya Kudumu Ya Utafiti Na Utoaji Fatwa, ikiongozwa na Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Aal Ash-Shaykh, Mufti mkuu wa Saudi Arabia, imeeleza Kamati hiyo kuwa mchezo huo unafanana na Kamari kwa sababu ya mashindano yaliyomo ndani yake ambayo yanahusisha pesa ambazo wachezaji wanaokusanya kadi za mchezo huo hubadilishana.

 

Kadhaalika, Kamati hiyo ya Kudumu ya Utoaji Fatwa, imeeleza kuwa dhana ya mchezo huo inaelekea imebuniwa kutokana na ile nadharia ya mageuzi ya Charles Darwin.

 

Kadi nyingi za mchezo huo zina takwimu ya nyota zenye ncha sita ambazo ni nembo ya kimataifa ya Kizayuni na Israel. Kadhaalika kuna nembo za msalaba katika kadi hizo, nembo za Kimasoni (freemasonry), na pia kuna nembo za Shinto au kami-no-michi ambayo ni dini ya kishirikina ya Kijapan ya kuabudu miungu wengi. Picha za nembo kama hizo zimejaa kwenye kadi za mchezo huo.

 

Kamati ya Kudumu ya Utafiti na Utoaji Fatwa, imeamua kuwa mchezo huo ni haraam na vilevile imeharamisha chumo lolote lile linalopatikana kutokana na mchezo huo kwa sababu ni chumo la kamari ambayo ni haraam.

 

Kadhaalika inaharamishwa kuuza na kununua, kwani hiyo ni njia inayopelekea kwenye yale yaliyoharamishwa na Allaah na Mtume Wake.

 

Na Kamati inawausia Waislamu wote wajihadhari na mchezo huo na kuwazuia watoto wao kutumia na kucheza mchezo huo ili kuhifadhi Dini yao na ‘Aqiydah yao na Akhlaaq zao.

 

Na Tawfiyq ni kutoka kwa Allaah.

 

Na Swalaah na Salaam ziwe juu ya Nabiy Muhammad na Aali zake na Swahaba zake.

 

Mwenyekiti:

 

‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaahi Aali Ash Shaykh (Hafidhwahu Allaah)

 

Wajumbe:

Swaalih bin Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

‘Abdullaah bin Ghudayaan (Rahimahu Allaah)

 

[Fatwa namba 21,758, tarehe 03.12.1421 H]

 

Share