Imaam Ibn Baaz: Vitabu Vya Tafsiyr Ya Qur-aan Vilivyo Bora

 

Vitabu Vya Tafsiyr Ya Qur-aan Vilivyo Bora

 

Imaam ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaahi bin Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ni Vitabu Vipi Vya Tafsiyr Ya Qur-aan Unavyoninasihi kudumu kuvisoma?

 

 

JIBU:

 

Bora zaidi katika hizo Tafsiyr kwa tunavyojua, ni Tafsiyr ya Ibn Jariyr na Tafsiyr ya Ibn Kathiyr na Tafsiyr ya Al-Baghawiy.

Lakini Tafsiyr ya Ibn Kathiyr ni bora zaidi ya hizo, kwa sababu imeshughulikia zaidi Ahaadiyth na imeshughulikia na kujali zaidi ‘Aqiydah ya Salafi; hii ni Tafsiyr nzuri japo iko kwa urefu.

Lakini tunakuusia uzingatie (kuisoma Qur-aan kwa mazingatio), achana na vitabu vya Tafsiyr (kwanza kabla hujaizingatia Qur-aan), tunakuusia usome Qur-aan kwa mazingatio na kuielewa, na waulize Wenye elimu juu ya yale yanayokutatiza (waulize) kwa njia ya simu, kwa njia ya maandishi (kuwaandikia), waulize yale ambayo yanakutatiza katika Aayah mbalimbali (za Qur-aan).

Na ikiwa una elimu ya kurejea Tafsiyr ya Ibn Jariyr au Ibn Kathiyr, au Al-Baghawiy kwa ajili ya faida, basi hilo ni (jambo) zuri.

 

Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz]

 

 

Share