Shaykh Fawzaan: Lipi Lenye Faida Zaidi; Kulingania Katika Da'wah Au Kutafuta Elimu Kwanza?

 

Lipi Lenye Faida Zaidi; Kulingania Katika Da'wah Au Kutafuta Elimu Kwanza?

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Ni jambo lipi katika haya mawili ni bora? Kutafuta elimu au kulingania watu kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kwa sababu nilisikia baadhi ya makundi yakisema: "Da'wah kwa ajili ya Allaah ni yenye faida kubwa kulikoni kutafuta elimu."

 

 

JIBU:

 

Kutafuta elimu ni jambo la mwanzo kabisa, kwa sababu haiwezekani mtu kuweza kuwalingania watu katika Dini ya Allaah mpaka awe na elimu; ama akiwa hana elimu basi hawezi kuwalingania watu katika Dini ya Allaah, na ikiwa atafanya (Da'wah) basi atakayokosea yatakuwa makubwa zaidi kuliko atakayopatia. Kwa hiyo, ni sharti kwa Mlinganiaji kuwa na elimu kabla ya kuanza kulingania watu; haya ni kutokana na kauli Yake Allaah:

 

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

Sema: “Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah, juu ya baswiyrah (nuru ya elimu, ujuzi, umaizi) mimi na anayenifuata. Na Subhaana-Allaah (Utakasifu ni wa Allaah), nami si miongoni mwa washirikina.” [Yuwsuf: 108]

 

Hata hivyo; kwa mambo ya wazi (yanayojulikana na kila mmoja) Inawezekana kwa mtu wa kawaida kulingania katika mambo hayo; kama kuamrisha Swalaah na kukataza kuipuuza (Swalaah), kuamrisha Swalaah ya Jamaa’ah (kwa wanaume), kuamrisha watoto kuswali; mambo haya yanafahamika kwa (wote); mtu wa kawaida na mtafutaji elimu.

 

Hata hivyo; mambo ambayo yanahitaji ufahamu na ujuzi kuhusu Halaal na Haraam na mambo ya Shirk na Tawhiyd, hayo basi lazima kutafutwe elimu katika hayo. Kwa ujumla, wote wanaosema ya kuwa; Kufanya Da'wah ni jambo lenye kunufaisha kulikoni kusoma, hao ni Jamaa’at At-Tabliygh na hao ni katika kundi potofu la uzushi la Kisufi.

 

 

[Al-Ijaabat Al-Faaswilah 'Alaa Ash-Shubuhaat Al-Haaswilah, uk. 20]

 

Share