026-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 026: إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 26-27: Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wao; ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” (Allaah) Huwapoteza kwayo (mfano huu) wengi na Huwaongoza kwayo wengi na wala Hawapotezi kwayo ila mafasiki.

 

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.  [Al-Baqarah: 26-27]

 

 

Sababun-Nuzuwl:  

 

Aayah hii imeteremshwa baada ya Allaah (سبحانه وتعالى) kupiga mifano kuhusu wanafiki katika kauli zifuatazo:

 

مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾

Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza (hivyo) hawaoni.  [Al-Baqarah: 17]

 

أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti, na Allaah ni Mwenye kuwazunguka kwa ujuzi Wake makafiri. [Al-Baqarah 19]

 

Wanafiki wakasema: “Allaah Ametukuka na Jalali zaidi imekuwaje apige mifano kama hii?” Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayaat hizi (2:26-27) mpaka kauli Yake: “… hao ndio wenye khasara.”.

 

Na Sa’iyd amesema kuwa Qataadah amesema: “Allaah (سبحانه وتعالى) Alipotaja nzi na buibui katika Kitabu Chake (Qur-aan), wapotofu wakasema: “Kwanini Allaah Ametaja vitu hivi?” Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah hiyo:

 

“Na Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo)…”   [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

Share