Hukmu Ya Kufanya Kazi Katika Kiwanda Cha Pombe

Hukmu Ya Kufanya Kazi Katika Kiwanda Cha Pombe

 

SWALI:

 

Naomba hukumu ya anayefanya kazi ktk kiwanda cha bia ilhali ni muislamu

 


 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Ni haramu Muislamu kufanya kazi katika kiwanda cha ulevi (bia na pombe zote). Na haifa hata Muislamu kushiriki kwenye mambo ya ulevi kwa aina yoyote ile kama kutangaza, kuhifadhi, kubeba, kusambaza n.k. Makatazo hayo yanapatikana kwenye ushahidi wa Hadiyth hii:

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelaani mambo kumi yanayohusiana na ulevi; mwenye kuukamua (kuutengeneza), Mwenye kutengenezewa, mnywaji, mbebaji, anayebebewa, anayeendesha (kuupeleka ulevi), muuzaji, anayekula thamani yake, anayenunua na anayeuza. [At-Tirmidhiy na Ibn Maajah)

Faidika zaidi katika kiungo kifuatacho:

Inafaa Kufanya Kazi Kunakouzwa Nguruwe Na Pombe Na Hawezi Kuswali Anakidhi Swalah Zote

Na Allaah Anajua zaidi

Share