144-Asbaabun-Nuzuwul: Kwa yakini Tumeona unavyogeuza geuza uso wako mbinguni...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 144: Kwa yakini Tumeona unavyogeuza geuza uso wako mbinguni....

 

 

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٤﴾

144. Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwepo (mkataka kuswali), basi elekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika wale waliopewa Kitabu bila shaka wanajua kwamba hivyo ni haki kutoka kwa Rabb wao. Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa wayatendayo.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivohadithia Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba:  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali akieleza uso wake Baytul-Maqdis (Palestina) kwa miezi kumi na sita au kumi na saba. Lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akipenda lakini alikuwa akitazamatazama mbinguni akitegemea amri ya Allaah (Ambadilishie Qiblah) ndipo ikateremka hii Aayah: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia…” (2: 144) [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo - Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share