014-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AL-MALIK, AL-MAALIK, AL-MALIYK

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

الْمَلِك – الْماَلِك - الْمَلِيك

AL-MALIK, AL-MAALIK, AL-MALIYK

 

 

 

Al-Malik:  Mfalme na mwenye mamlaka.

 

Al-Maalik: Mwenye kumiliki.

 

Al-Maliyk: Mfalme Mwenye nguvu zote daima

 

Majina hayo matatu ni ya Allaah ('Azza wa Jalla) Ambaye Mwenye sifa ya ‘Mulk’ (Mwenye kumilki): Anamiliki, Ufalme, mamlaka, nguvu, taadhima, utukufu, enzi, na utukufu. Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni Pekee Mwenye kutawala na kumiliki vilivyoko mbinguni na ardhini na vilivyoko baina yake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢﴾

Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, Anahuisha na Anafisha, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-Hadiyd: 2]

 

Al-Malik imetajwa mara tano katika Qur-aan:

 

فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۗ وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾

Basi Ametukuka Allaah kwa ‘Uluwa, Mfalme wa haki. Na wala usiiharakize Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabla haikumalizwa kufunuliwa Wahy kwako. Na sema: “Rabb wangu! Nizidishie elimu.” [Twaahaa: 114]

 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ  

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme.[Al-Hashr: 23]

 

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾

Sema: Najikinga na Rabb wa watu.

 

مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾

Mfalme wa watu. [An-Naas: 1-2]

 

فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ﴿١١٦﴾

Basi Ametukuka Allaah Mfalme wa haki. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Rabb wa ‘Arsh tukufu.  [Al-Muuminuwn: 116]

 

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾

Vinamsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Mfalme, Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Jumu’ah: 1]

 

Al-Maalik imetajwa mara mbili katika kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾

Mfalme wa siku ya malipo. [Al-Faatihah: 4]

 

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ

Sema: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye [Aal-‘Imraan: 26]

 

 

Ama Al-Maliyk imetajwa mara moja katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ ﴿٥٤﴾

Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na mito.  

 

فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍ ﴿٥٥﴾

Katika makao ya haki kwa Mfalme Mwenye Nguvu zote, Mwenye Uwezo wa juu kabisa. [Al-Qamar: 54-55]

 

 

Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Ndiye Al-Malik, Al-Maalik na Al-Maliyk: Mwenye Ufalme wote, Mwenye kumiliki yote, Mwenye kuhimidiwa kwa yote. Mambo yote yapo chini Yake na Yanarejea Kwake.  Istawaa katika ‘Arshi Yake (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). Yuko juu ya viumbe Vyake vyote, hakijifichi chenye kujificha katika ardhi wala katika mbingu.

 

Allaah (‘Azza wa Jalla) Anapanga Pekee mamlaka Yake. Anatoa na kuzuia, Anakirimu, Anatukuza na Anadhalilisha, Anaumba na kuruzuku, Anaamrisha na Anakataza, Anafisha na kuhuisha, Anakadiria na Anahukumu. Anaingiza usiku kwa mchana, na Anaingiza mchana kwa usiku. Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾

Sema: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾

Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku; na Unatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Unatoa kilicho mfu kutokana na kilicho hai na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu.  [Aal-‘Imraan: 26-27]

 

Anatawala Atakavyo, Anamiliki Atakayo. Ni Muweza hakuna mwenye kushindana Naye katika mamlaka Yake, wala hakuna mwenye kuweza kumpinga. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾

Hakika amri Yake Anapotaka chochote hukiambia: “Kun! (Kuwa), nacho huwa.”

 

فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾

Basi Subhaanah! Utakasifu ni wa Ambaye Mkononi Mwake kuna ufalme wa kila kitu, na Kwake mtarejeshwa. [Yaasiyn: 82-83]

 

Ibn Jariyr amesema: “Ni Mfalme Ambaye hakuna ufalme juu Yake wala chochote isipokuwa kiko kwenye mamlaka Yake.” [Jaami’ Al-Bayaan (28/36]

 

Na Ibn Al-Qayyim amesema: “Mfalme wa haki. Yeye Ambaye Anaamrisha na kukataza na Anasarifu Atakavyo kwa viumbe Vyake kwa kauli na Amri Zake, na hii ndio tofauti baina ya Al-Malik na Al-Maalik.

 

Hivyo basi Al-Maalik ni Mwenye kufanya Atakavyo kwa vitendo Vyake. Na Al-Malik ni Mwenye kutenda Atakavyo kwa vitendo Vyake na amri Zake Na Rabb (Ta’aalaa) ni Mfalme wa ufalme basi Hufanya Atakavyo kwa vitendo Vyake na amri Zake.” [Badaai‘u Al-Fawaaid (4/165)]

 

 

Na Ibn Kathiyr amesema kuhusu kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ  

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme… [Al-Hashr: 23]

 

Kwa maana: Ni Mfalme wa kila kitu Anayefanya Atakavyo bila ya mwenye kumkataza au kumpinga. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Majina ya Allaah:

Al-Malik, Al-Maalik, Al-Maliyk

 

1.     Ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni Mfalme wa wafalme, na hakuna anayeweza kushindana Naye kwa lolote, wala hakuna mshirika, na Ndiye rejea yetu na matarajio yetu, hatuwezi kutoshelezwa na asiyekuwa Yeye. Hivyo hakuna haja ya kuogopa, wala kutarajia asiyekuwa Yeye, wala kumpenda asiyekuwa Yeye, wala kumtegemea asiyekuwa Yeye, kwani mwenye kumtegemea na kumuogopa Yeye Al-Malik, Al-Maalik, Al-Maliyk, basi atakuwa chini ya uangalizi Wake.  

 

 

2.     Haipasi kujiita Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) yanayomhusu Yeye Pekee kama haya yenye kuanzia na ‘AL’ (Al-Malik) au ‘Maalik Al-Amlaak’ (mfalme wa wafalme) kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametahadharisha:

 

((أَغْيَظُ رَجُلٍ عَلَى اللَّهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَخْبَثُهُ وَأَغْيَظُهُ عَلَيْهِ رَجُلٌ كَانَ يُسَمَّى مَلِكَ الأَمْلاَكِ لاَ مَلِكَ إِلاَّ اللَّهُ))

Mtu anayechukiza kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni muovu kabisa na anayechukiza mno kuliko wote. Kwake ni mtu aliyekuwa akijiita: “Maalik Al-Amlaak” (Mfalme wa wafalme). Kwani hakuna mfalme isipokuwa Allaah. [Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika Muslim, Kitaab Al-Iymaan]

 

 

3.     Wafalme wa duniani wana mamlaka ya watu wao duniani tu na ni mamlaka ya muda mfupi tu. Ama Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni Al-Malik, Al-Maalik; Al-Maliyk, Mfalme wa wa wafalme wote, na Mwenye ufalme wa kudumu. Ni Mfalme wa duniani na Aakhirah. Siku watakapofishwa viumbe wote Atabakia Maalikul-Mulk (Mfalme wa wafalme). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَوْمَ هُم بَارِزُونَ ۖ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ ۚ لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ۖ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ ﴿١٦﴾

Siku watakayotokeza wao, hakitofichika kitu chochote chao kwa Allaah. “Ufalme ni wa nani leo?” (Allaah Mwenyewe Atajijibu): “Ni wa Allaah Pekee Mmoja, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Asiyepingika.” [Ghaafir: 16]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا ﴿٢٥﴾

Na Siku itakayoraruka mbingu kwa mawingu; na Malaika watateremshwa mteremsho mkubwa wa mfuatano.

 

الْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ لِلرَّحْمَـٰنِ ۚ وَكَانَ يَوْمًا عَلَى الْكَافِرِينَ عَسِيرًا ﴿٢٦﴾

Ufalme wa haki Siku hiyo utakuwa ni wa Ar-Rahmaan; Mwingi wa Rahmah.  Na itakuwa ni siku ngumu kwa makafiri. [Al-Furqaan: 25-26]

 

Na katika Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((يَقْبِضُ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى الأَرْضَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَطْوِي السَّمَاءَ بِيَمِينِهِ ثُمَّ يَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ أَيْنَ مُلُوكُ الأَرْضِ))

((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Ataikamata ardhi Mkononi na Atazikunja mbingu kwa Mkono Wake wa kulia kisha Atasema: Mimi Ndio Mfalme! Wako wapi wafalme wa duniani?)) [Hadiyth ya Abuu Hurayrah ameikusanya Al-Bukhaariy katika Kitaab At-Tafsiyr, Kitaab At-Tawhiyd, Kitaab Ar-Raqaaiq na Muslim katika Kitaabu Swiffatil-Qiyaamah Wal-Jannati Wan-Naari]

 

 

4.     Kwa mwenye madaraka, au mamlaka au cheo chochote kile duniani, au umiliki wa chochote kile, awe mnyenyekevu kwa walio chini yake kwa kuzingatia kuwa Yuko Al-Malik na Al-Maliyk Ambaye Ana mamlaka juu yake. Hivyo basi unapohukumu, uhukumu kwa haki bila ya uonevu. Unapotoa, toa bila ya kupendelea, na wala usitakabari bali ukhofie kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

يَطوي اللهُ عزَّ وجلَّ السَّماواتِ يومَ القيامةِ. ثمَّ يأخذُهنَّ بيدِه اليُمنَى. ثمَّ يقولُ: أنا الملِكُ. أين الجبَّارون؟ أين المُتكبِّرون؟ ثمَّ يَطوي الأرضين بشمالِه. ثمَّ يقولُ: أنا الملِكُ. أين الجبَّارون؟ أين المُتكبِّرون؟

Allaah ‘(Azza wa Jalla) Atakunja mbingu zote Siku ya Qiyaamah kisha Atazikamata Mkononi Mwake wa kuume Atasema: Mimi Ndiye Mfalme. Wako wapi waliojifanya majabari? Wako wapi waliotakabari? Kisha Atakunja ardhi mbili kwa Mkono Wake wa kushoto Atasema: Mimi Ndiye Mfalme, wako wapi waliojifanya majabari. Wako wapi waliotakabari?)) [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) katika Muslim 2788, na Ibn Maajah, na Abuu Daawuwd]

 

 

5.     Kusoma adhkaar zilizothibiti zenye kutajwa Majina haya ya Allaah au Sifa Zake mfano:

اللّهُـمَّ أَنْتَ المَلِكُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْت، أَنْتَ رَبِّـي وَأَنـا عَبْـدُك، ظَلَمْـتُ نَفْسـي وَاعْـتَرَفْتُ بِذَنْبـي فَاغْفِرْ لي ذُنوبي جَميعاً إِنَّـه لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إلاّ أَنْت،

Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illa Anta. Anta Rabbiy wa ana ‘abduka, dhwalamtu nafsiy wa’-taraftu bidhanbiy faghfir-liy dhunuwbiy jamiy’an innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta

 

Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe Ndiye Rabb wangu na mimi ni mja Wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nighufurie madhambi yangu yote, hakika haghufurii madhambi, ila Wewe [Miongoni mwa du’aa za kufungulia Swalaah]

 

Pia:

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ المُلكُ ولهُ الحَمْد، يُحيـي وَيُمـيتُ وهُوَ على كُلّ شيءٍ قدير.  

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu, Yuhyi wa Yumiytu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr

Hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah, ni Mmoja Pekee, Hana mshirika. Ni wake Ufalme, na kuhimidiwa ni Kwake, Anahuisha, Anafisha, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.

 

 

6.     Tafakari Aayah katika Suwratul-Faatihah unayoisoma katika kila Swalaah zako:

 

مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾

Mfalme wa siku ya malipo.

 

Kwamba umesimama mbele ya Al-Maalik na Mfalme wa wafalme duniani na kwamba utasimamishwa mbele Yake tena Siku ya Qiyaamah kulipwa mema uliyoyatenda na kuhesabiwa maovu uliyoyatenda wala hakuna cha kufichikia siku hiyo!  

 

  يَوْمَ هُم بَارِزُونَ ۖ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ ۚ لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ۖ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ ﴿١٦﴾

Siku watakayotokeza wao, hakitofichika kitu chochote chao kwa Allaah. “Ufalme ni wa nani leo?” (Allaah Mwenyewe Atajijibu): “Ni wa Allaah Pekee Mmoja, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Asiyepingika.”

 

الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۚ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٧﴾

Leo kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyachuma, hakuna dhulma leo!  Hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.

 

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْآزِفَةِ إِذِ الْقُلُوبُ لَدَى الْحَنَاجِرِ كَاظِمِينَ ۚ مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ ﴿١٨﴾

Na waonye Siku inayokurubia sana pale nyoyo zitakapofikia kooni wamejaa huzuni na majuto. Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, na wala mwombezi anayetiiwa. [Ghaafir: 16-18]

 

Tafakari pia Aayah katika Suwratul-Infitwaar [13-19]

 

 

7.     Tafakari neema za Jannah Anazotuahidi Allaah (‘Azza wa Jalla) huko. Kwa hiyo, tenda mema na jiepushe na maovu uipate Jannah. Pale utakapoingia Jannah ukafunguliwa milango yake na Malaika wakakupokea kwa Salaamun ‘Alaykum! Ukaanza kuona Anayoyamiliki Al-Maalik, huko: 

وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا ﴿٢٠﴾

Na utakapoona huko, utaona neema na milki adhimu. [Al-Insaan: 20]

 

 

 

Share