Shaykh Fawzaan: Kuhifadhi Nguo Za Maiti

 

Kuhifadhi Nguo Za Maiti  

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, inajuzu kuhifadhi nguo za maiti? Na ikiwa haijuzu, basi ni lilo bora kuzifanya?

 

 

JIBU:

 

Inafaa kunufaika na nguo za maiti kwa atakayezivaa katika familia yake au kuzigawa nguo kwa atakayezivaa kwa wanaozihitajia wala zisitupwe.

 

Kwa vyovyote vile, hizo ni sehemu ya mirathi ikiwa ni zenye thamani basi zihesabiwe kuwa ni sehemu ya mirathi inayowastahiki warithi wake. 

 

Kuzihifadhi kwa ajili ya kumbukumbu haijuzu na haipasi na huenda ikawa ni haraam ikiwa niyyah ya kufanya hivyo ni kutabarruk (kutafuta baraka) kwa nguo hizo. Na hivyo ni kupoteza pesa kwa sababu zinapaswa kutumiwa si kuzihifadhi bila ya kuzitumia. 

 

 

[Shaykh Fawzaan, Al-Muntaqaa (2/287-288)]

 

 

Share