Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Nguo Za Aliyefariki Kuvaliwa Na Ahli Wake

Nguo Za Aliyefariki Kuvaliwa Na Ahli Wake

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, inafaa ahli wa maiti kutumia nguo alizoziacha aliyefariki?

 

 

JIBU:

 

Na’am. Ikiwa mtu amefariki kila alichokimiliki kinakuwa ni mali ya warithi wake kama nguo, fanicha, vitabu, vitu vya kuandikia, meza, viti na kila kitu hata kilemba alichokuwa akivaa vinakuwa ni mali ya warithi. Itakapokuwa ni mali ya warithi, basi wao wanaweza kusarifu wapendavyo kama vile wanavyosarifu mali zao.

 

Ikiwa hao warithi ni watu wazima wenye akili zao na wakiamua kuwa nguo za maiti apewe mmoja wao na azivae hakuna ubaya. Ikiwa watakubaliana kuzitoa swadaqah pia hakuna ubaya.

 

Na ikiwa wote watakubaliana kuizuza hakuna ubaya. Hizo ni mali zao na wana haki kusarifu wapendavyo kama mtu anavyosarifu mali zake apendavyo.

 

 

[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn, Fataawa Nuwr ‘Alaa Ad-Darb]

 

 

Share