Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Bid'ah Inayomtoa Mtu Katika Uislamu Na Bid’ah Ya Ufasiki

Bid’ah Inayomtoa Mtu Katika Uislamu Na Bid’ah Ya Ufasiki

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ni ipi bid’ah inayomtoa mtu katika Uislamu na ipi bid’ah isiyokuwa hiyo?

 

 

JIBU:

 

Kidhibiti katika (suala) hili ni: Ikiwa bid’ah inapingana na Uislamu au inalazimu kuufanyia uadui Uadui Uislamu, basi hiyo ni bid’ah yenye kukufurisha (kupelekea kwenye ukafiri).

 

Ama ikiwa si kama hivyo, basi itakuwa ni bid’ah yenye kupelekea kwenye ufasiki.

 

Na miongoni mwa bid’ah isiyokufurisha ni kile walichozua watu katika matamshi maalum ya Adhkaar, au wakaweka nyakati maalum kwa ajili ya Adhkaar (nyakati) ambazo (mafunzo ya) Sunnah hayajaweka au kupangilia (nyakati hizo).

Ingawa (Adhkaar) kiasili ni jambo lipo kishariy’ah, lakini wao wamefunga kwa zama ambayo Qur-aan na Sunnah haijazifunga (hizo Adhkaar).

 

Na ama zile bid’ah zenye kukufurisha ambazo zinazolazimu kumtia mapungufu Muumba (Allaah), au kumtia mapungufu Rasuli, au kutia mapungufu walioinukulu (walioibeba na kuwafikishia wengine) shariy’ah kama vile Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum); basi hizi ni bid’ah zenye kukufurisha.

 

Kilicho muhimu (kukifahamu), kile chenye kuutengua Uislamu miongoni mwa bid’ah, basi bid’ah hiyo ni yenye kukufurisha, na kile kisichoutengua Uislamu basi hiyo ni bid’ah isiyo ya kukufurisha.

 

 

[http://binothaimeen.net/content/11682] 

 

 

Share