Kubadilisha Jina La Baba Inajuzu?

 

SWALI

asalam alaikum warahmatu llahi, baada ya salam na kumshukuru aza wajalah kwa rehma zake na mtume wetu mohammad (s.a.w) ninapenda kushukua nafasi hii kuuliza suala kuhusu jina la baba yako, kwani limekua linanitatiza tokea nilipoambiwa na wenzangu kua inasemekana kidini huruhusiwi kubadilisha jina la baba.  Mimi ninaishi UK with a Permanent Resident as a Tanzanian Citizen, lakini tokea tumeowana na mume wangu registration Office jina langu nimebadilisha yaani jina langu la mwanzo kama kawaida halafu limefaatiya la baba angu ikisha ndio la mumewangu kwa sababu ya mabo ya nyumba nakadhalika.  Suala ni hili Jee hapa nitakua nimeondosha jina na Babu yangu nikaweka la mume wangu inasihi hiii kwa mafundisho ya dini na sheria za kiislamu?, naomba ufumbuzi wako kwani ikibidi niweze kujua nini nafanya.     

 







JIBU:

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad:

Uislamu umekataza kubadilisha jina la baba na kutumia jina lolote jengine kama kutumia jina la mume. Anasema Allaah سبحانه وتعالى  

 

((ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ))

((Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu)) [Al-Ahzaab: 5]

 

Aayah hii ileteremshwa baada ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  alipomchukua Zayd bin Haarith na kumfanya ni mtoto wa kupanga (adoption) ambaye baada ya hapo aliitwa Zayd bin Muhammad. Allaah سبحانه وتعالى Akataka kuondosha mila hiyo ya kumbadilisha mtu jina la baba yake, kwa hiyo baada ya kuteremka Aayah hii, akarudia kuitwa kwa jina lake la asili Zayd bin Haarith.

 

Na ndio maana hata kama Kafiri akibadilisha Dini, anaweza kubadilisha jina lake tu, na si jina la baba.

 

Na tabia ya mke kubadilisha jina kutumia jina la mume, mfano kuitwa Mrs Juma, ni tabia zisizolingana na maadili na mafundisho ya Kiislam kabisa! Na kama mwanamke anataka kutumia jina lisilo lake, basi anaweza kutumia kun-yah (nickname) kwa umama wa mtoto wake, mfano Mama ‘Aliy au Ummu ‘Aliy n.k.

 

Kufanya hivyo vile vile kuna madhara yake. Kwanza tabu ya kubadiisha pasipoti na vyeti vinginevyo kwa ajili ya utambulisho katika idara za serikali.

 

Pili, inapotokea kifo cha mume au talaka, inabidi mke arudie kubadilisha pasipoti na vyeti vyake vyote vingine kuweka jina la baba badala ya jina mume, hivyo ni usumbufu unaompotezea mtu fedha na wakati wake.

 

Kwa hiyo Muislamu ni bora kubakia katika amri na mafunzo ya dini yake ili kupata ridha ya Mola wake na pia kujiepusha na usumbufu mbali mbali.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share