135-Aayah Na Mafunzo: Dini Ya Nabiy Ibraahiym Ndio Dini Ya Kiislamu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Dini Ya Nabiy Ibraahiym Ndio Dini Ya Kiislamu

 

 

 

وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا ۗ قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wakasema: “Kuweni Mayahudi au Manaswara mtaongoka.” Sema:  “Bali (tunafuata) mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na wala hakuwa katika washirikina.” [Al-Baqarah: 135]

 

 

Mafunzo:

 

Amesimulia Ibn Umar (رضي الله عنهما) kwamba: Zayd bin ‘Amr bin Nufayl, alitoka kuelekea Sham, akiulizia kuhusu dini ili aifuate. Akakutana na mwanazuoni wa ki-Yahudi, akamuuliza kuhusu dini na akasema: Mimi huenda nikaingia dini yenu, basi nielezee. Akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika ghadhabu za Allaah. Akasema Zayd: Mimi hakuna ninachokikimbia ila ghadhabu za Allaah, wala sivumilii ghadhabu za Allaah kwa kitu chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema (mwanachuoni wa ki-Yahudi): Sijui ila Dini iliyotakasika, akasema Zayd: Ni (dini) ipi hiyo iliyotakasia? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara, wala haabudu ila Allaah. Akatoka Zayd akakutana na mwanazuoni wa ki-Naswara, akamuuliza kama vile (alivyomuuliza Myahudi), akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika laana za Allaah. Akasema: Mimi hakuna nnachokimbia ila nakimbia laana za Allaah, wala sivumilii laana za Allaah wala ghadhabu zake kwa chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema: sijui ila (Dini) iliyotakasika. Akasema: Ni ipi hiyo (Dini) iliyotakasika? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara wala haabudu ila Allaah. Basi Zayd alipoona maneno yao kuhusu Ibraahiym  (عليه السلام)  aliondoka sehemu hiyo, na alipokuwa nje aliinua mikono yake akasema; “Ee Allaah mimi nashuhudia niko katika Dini ya Ibraahiym.” [Al-Bukhaariy (3827)]

 

Share