187-Aayah Na Mafunzo: Ruhusa Ya Kula Na Kunywa Usiku Wa Ramadhwaan

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Ruhusa Ya Kula Na Kunywa Usiku Wa Ramadhwaan  

 

www.alhidaaya.com

 

 

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku. Na wala msiwaingilie hali ya kuwa nyinyi wenye kukaa i’tikaaf Misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.

 

Maswahaba walitatanishwa na kushindwa kuelewa maana ya neno uzi mweupe kutokana na uzi mweusi.” ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Ilipoteremshwa Aayah: mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku)”, Nilichukua uzi mmoja mweupe na mmoja mweusi nikaweka chini ya mto wangu lakini haikunibainikia. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلمasubuhi nikamwelezea. Akasema: “Hakika hiyo (imekusudiwa) ni kiza cha usiku na weupe wa Alfajiri” [Al-Bukhaariy Na Muslim]

 

 

Share