203-Aayah Na Mafunzo: Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi Masiku Ya Tashriyq

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi Masiku Ya Tashriyq

 

 

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٠٣﴾

203. Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. Atakayeharakisha kuondoka katika siku mbili, basi hakuna dhambi juu yake; na atakayetaakhari basi hakuna dhambi juu yake; kwa mwenye kuwa na taqwa. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.

 

 

Mafunzo:

 

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Siku za kuhesabika ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na siku zinazojulikana ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Al-Qurtwubiy: 3.3]

 

 

 

Share