222-Aayah Na Mafunzo: Hukmu Ya Haramisho La Kujimai Na Mwanamke Akiwa Katika Hedhi Au Nifaas Ni Moja

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Hukmu Ya Haramisho La Kujimai Na Mwanamke Akiwa Katika Hedhi Au Nifaas Ni Moja

 

www.alhidaaya.com

 

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah.” Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.

 

 

Mafunzo:

 

Kuruhusiwa kufanya kila jambo isipokuwa kujimai.

 

عن  أنس رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ الْيَهُودَ كَانُوا إِذَا حَاضَتِ الْمَرْأَةُ؛ لَمْ يُؤَاكِلُوهَا. فَقَالَ النَّبِيُّ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اصْنَعُوا كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ النِّكَاحَ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mayahudi walikuwa hawali na mwanamke anapokuwa katika hedhi. Lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Fanyeni naye kila jambo isipokuwa kujimai)) [Muslim]

 

Haramisho la kumuingilia:

 

Mwenye kumuingia mwenye hedhi au mwanamke kwenye dubur (uchi wa nyuma) au kumwendea mtabiri na kumuamini kwa anayosema basi amekufuru kwa aliyoteremshiwa Muhammad.” [Swahiyh At-Tirmidhiy (135), Swahiyh Ibn Maajah (528), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (7/1130)].

 

Imaam Ibn Taymiyyah amesema:

 

"Kuwaingilia wenye nifasi ni kama kumwingilia mwenye hedhi, na hilo ni haramu kwa makubaliano ya Maimaam. [Al-Fataawaa (21/624)]

 

 

Share