Mkopo Wa Nyumba Wa Benki (Mortgage) Ni Halali?
SWALI
Assalaam Alykum,
Jina langu ni ………. na punde tu nimejaza uanachama wa Alhidaaya ili niwe napokea jarida la Alhidaaya. Kwa bahati nzuri ni miongoni mwa Waislamu waishio ughaibuni na kwa sasa niko Marekani. Nimejaaliwa kuoa muislamu aliyezaliwa na kulelewa katika maisha haya na Alhamdulillah namshukuru Allah kwani kuwa kwetu pamoja kumeniongeza imani na kujua mengi. Allah aidumishe ndoa yetu na tuendelee kupata kizazi chema.
Katika kutafuta maisha na kujitayarishia makazi ya hapa nimepata ushawishi wa karibu wa kutaka kununua nyumba. Hasa kwa vile ikhwaan wengi ninao wafahamu hapa wameingia kwenye biashara hiyo ya kujitafutia makazi wao na ahli zao. Baada ya maswali mengi niliyowauliza nimeona kuwa katika ununuaji wa nyumba hizi kuna riba kubwa sana na kwa ufupi hili limenirudisha nyuma kwani kwa ninavyofahamu mimi na familia yangu na waislamu wengi ninaowafahamu riba ni riba tu hata ikiwa ndogo au kubwa.
Wengi niliozungumza nao majibu
Swali langu liko hapa je
Nashukuru kwa muda wenu na natanguliza shukrani za dhati.
Nduguyo katika Uislam
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kubwa
Ni hakika kuwa Uislam umeruhusu kukuzwa kwa
((Enyi mlioamini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe)) (
Lakini Uislam umeziba njia mbele ya kila anayejaribu kuikuza
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameteremsha ayah kali
Hukumu ya riba ni kuwa imeharamishwa kwa kauli ya Aliyetukuka: ((Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni
Pia amesema Mtume wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Allaah Amelaani mwenye kula riba, mwenye kuitoa, mashahidi wake na mwandishi wake)) (Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaaiy na Ibn Maajah).
Amesema tena (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Dirhamu moja ya riba anayokula mtu naye anajua ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara 36)) (Ahmad kwa Isnadi sahihi).
Na pia: ((Riba ina milango 73, iliyo nyepesi zaidi ni mtu kumuoa mamake)) (al-Haakim, naye akaisahihisha).
Na kauli yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Jiepusheni na maangamivu saba)). Pakasemwa: ((Ewe Mjumbe wa Allah! ni yepi hayo?)) Akasema: ((kula riba)) (al-Bukhaariy na Muslim).
Hekima ya kuharamishwa:
Kwa hekima zilizo dhahiri katika kuharamishwa riba ni ziada kwa hekima za kijumla katika amali zote za kisheria nao ni mtihani wa Imani kwa mja katika utiifu wake. Na katika
1. Kuhifadhi
2. Inamtaka mtu achukue mali ya mwenzake bila kumpa chochote badili yake, kwani mwenye kutoa dirhamu moja apate mbili huwa amejipatia dirhamu moja zaidi bila ya kutoa chochote.
3. Kutegemea riba kunawazuia watu wasishughulike na kutafuta mapato. Huu ni katika upande wa kiuchumi.
4. Huondosha hisani iliyopo baina ya watu kutokana na kukopeshana. Huu ni upande wa akhlaaq na tabia njema.
5. Riba inawaendeleza matajiri kuzidi kuwanyonya masikini, hivyo tajiri huzidi kuwa tajiri na masikini huzidi kuwa masikini.
6. Kufunga njia za kueneza uadui na mashaka baina ya Waislam walio ndugu na kuwasababishia ghadhabu na chuki baina
7. Kumuepusha Muislam katika kuzalisha
8. Kumuepusha Muislamu na kinachompelekea katika kuhiliki. Anapokula riba anaingia katika dhulma na mwisho wake unakuwa mbaya
9. Kukopesha bila riba kunafungua milango ya wema baina ya Waislamu, hivyo kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: ((Na saidianeni katika wema na ucha Mungu, wala msisaidiane katika dhambi na uadui)) (5: 2).
Tufahamu kuwa haramu ni haramu, ndio Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Kileweshacho wingi wake basi uchache wake ni haramu)) (Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy).
Hivyo, riba inapokuwa kidogo au nyingi yote inaingia katika uharamu ambao Waislam hawafai kuingia ndani yake.
Sisi wanaadamu tumeumbwa tukiwa dhaifu
Hakika ni kuwa baadhi ya Waislam wameingia katika riba pindi wanapochukua mkopo kutoka benki au taasisi nyengine yoyote inayotoa mikopo kwa riba ili kufanyia shughuli yoyote, au kununua nyumba kwa udundulizi au rehani (mortgage). Katika hilo wamechukua fatwa kutoka kwa wenye kusahilisha na kudai kuwa hilo linaruhusiwa kwa wasiokuwa na nyumba kwa sababu za dharura na kwa sababu eti kulipa kodi ya nyumba kunamdhuru Muislam maana pesa yake inapotea lakini mogeji pesa inahifadhika!!
Wakalinganisha (Qiyaas)
Hakika ni kuwa kuna watu wanaishi hata katika mahema. Na kufanya hivyo ni kheri kwake mtu kuliko kuchukua mkopo wa riba na kujiweka katika kupigana vita na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na Mtume Wake.
Huenda huyu mdaiwa akashindwa kulipa deni, hivyo deni kuzidi juu ya matarajio yako. Benki huwa hazitaki kusikia kuwa mimi sasa sina kazi, au mshahara umepunguzwa au nilitumia pesa kwa shida na matatizo mengine. Hayo na yako, wao wanataka pesa mlizosikilizana kwa kila mwezi. Pesa hizo utazitowa wapi ni shauri yako. Tatizo hilo likitokea basi ufakiri utazidi, pia huenda ukauza nyumba hiyo au benki ikaiuza na faida juu yake na pesa zote zinakuwa ni zao nawe unaruka patupu. Pesa zote zinakwenda benki au kwa ambayo ndio ilikukopesha au ilisimamia mkataba wako na mwenye nyumba.
Nchi kadhaa kama Phillipine, Mexico, Thailand na kadhalika uchumi wao uliharibika kwa sababu ya kuchukua mikopo ya riba kutoka kwa Benki ya Dunia au IMF, kisha wakashindwa kulipa. Na wangapi tumewaona waliochukua mikopo kwa ajili ya kuendesha biashara au kununua nyumba, biashara ikaharibika na kuondoka au nyumba kuikosa. Mfano hai ni hivi karibuni Muislam mwenye mabasi marufu Tanzania wadeni wake waliyashika mabasi yake mazuri kwa sababu ya kutolipa kwa muda ufaao, hivyo ikasababisha biashara yake kurudi nyuma
Benki mara nyingi haitoi mkopo mpaka uwe na dhamana kwa sababu wao hawakubali kupata hasara kwa namna yoyote ile. Katika hilo unafaa uweke kwao hati ya nyumba nyengine, log book ya gari au kitu chochote chenye thamani ya mkopo unaochukua. Ukikosa tu kulipa kwa muda mlioandikiana ulichoweka kwao rehani kinauzwa ili warudishe deni lao. Hii ni dhulma ya hali ya juu kwani wewe huwa umelipa baadhi ya deni na kushindwa kwako kulipa basi kutapelekea kila kitu chako ulichowekesha kitoweke.
Kuhusu kipande cha mwisho kuwa tutafanya nini katika hali hiyo? Kitu cha kwanza ni kuwa ni lazima Waislam sehemu hiyo mushikamane na kuangalia tatizo
· Kuanzisha vyama vya co-operative na wakawa wanatoa ada ya kila mwezi au mwaka kiwango ambacho mtaridhiana. Baada ya muda mmoja anaweza kukopesha pesa za kiwango ambacho yeye ataka kufanya jambo Fulani. Akichukua mkopo atakuwa analipa polepole pamoja na ada ya kila mwezi. Kwa njia hii wanaweza kufanya mengi kwa uwezo wa Allaah Aliyetukuka.
· Kuweza kukaa na matajiri Waislam na kuwaeleza umuhimu wa kujenga nyumba na kuweza kuwauzia Waislam. Hili linafanyika huko
· Kikozi, japokuwa pesa zinazopatikana zinakuwa ni kidogo isipokuwa muwe watu wengi au munalipa ada ya kila mwezi kubwa zaidi
· Au njia nyengine yoyote ya halali.
Na Waislam wakiwa na moyo wa kuepuka haramu basi Allaah Aliyetukuka huwatolea njia ya kuweza kuondoka katika matatizo. Allaah Aliyetukuka Anasema: ((Na anayemcha Allaah Humtengezea njia ya kutokea. Na Humruzuku kwa njia asiyotazamia. Na anayemtegemea Allah Yeye humtosha)) (66: 2 - 3).
Na Allah Anajua zaidi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


