236-Mataa'u (Kiliwazo, Kitoka Nyumba, Masurufu) Ya Kumpa Mke Anayetalikiwa

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah

 

 Mataa'u  au Mut'ah Atw-Twalaaq (Kiliwazo, Kitoka Nyumba, Masurufu)

Ya Kumpa Mke Anayetalikiwa

 

www.alhidaaya.com

 

 

لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٣٦﴾

236. Hakuna dhambi kwenu mkiwatalaki wanawake ambao hamkuwagusa au kuwabainishia kwao mahari. Wapeni kiliwazo kwa mwenye wasaa kadiri ya uwezo wake na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake. Maliwaza kwa mujibu wa ada, ni haki kwa wafanya ihsaan.

 

 

وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٧﴾ 

237. Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa na mkawa mmeshawabainishia kwao mahari, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha isipokuwa wakisamehe au asamehe yule ambaye fungamano ya ndoa liko mikononi mwake. Na mkisamehe ni ukaribu zaidi ya taqwa. Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuona.

 

 

Mafunzo:

 

Mukhtasari Wa Mataa'u  au Mut'ah Atw-Twalaaq (Kiliwazo, Kitoka Nyumba, Masurufu) Ya Kumpa Mke Anayeachwa

 

Hali Ya 1:

Nikaah imefungwa, maingiliano hayakutendeka, mahari hayakubainishwa.

Hukmu Yake: Kadiri ya uwezo wa mume na pia mwanamke hahitaji kukaa eda.

 

Hali Ya 2:

Nikaah imefungwa, maingiliano hayakutendeka, mahari yamebainishwa.

Hukmu Yake: Nusu Ya mahari yaliyobainishwa. Pia hana haja ya kukaa eda.

 

Hali Ya 3:

Nikaah imefungwa, maingiliano yametendekea, mahari yamebainishwa.

Hukmu yake: Apewe mahari kamili.

 

Hali ya 4:

Nikaah imefungwa, maingiliano yametendeka, mahari hayakubainishwa.

Hukmu yake: Apewe mahari yanayolingana na mahari waliopewa wanawake wengine katika familia yake.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share