238-Aayah Na Mafunzo: Umuhimu Wa Kuhifadhi Swalaah Ya Alasiri

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

 

Umuhimu Wa Kuhifadhi Swalaah Ya Alasiri

 www.alhidaaya.com

 

 

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.

 

 

Mafunzo:

 

Umuhimu wa Swalaah ya ‘Alasiri: Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kupitwa na Swalaah ya Alasiri ni kama amedhulumiwa watu wake na mali yake.” [Al-Bukhaariy (552)]

 

 

 

Share