276-Aayah Na Mafunzo: Ribaa Haizidishi Bali Inapunguza Na Kufilisi Mali

Al-Baqarah

Ribaa Haizidishi Bali Inapunguza Na Kufilisi Mali

 www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:)

 

 يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾

276. Allaah Huifuta baraka (mali ya) ribaa na Huzibariki swadaqah. Na Allaah Hapendi kila kafiri apapiae madhambi.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote anayetoa swadaqah inayolingana na tende, kutokana na mali ya halali, na Allaah Hakubali isipokuwa kilicho kizuri na safi, basi hakika Allaah Hukipokea kwa Mkono Wake wa kulia kisha Hukiinua kwa mtoaji, kama mtu anayemfuga mwanafarasi wake, mpaka inakuwa (swadaqah) hiyo kama mlima.” [Muslim katika kitaab cha Zakaah]

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakithirishi yeyote katika ribaa ispokuwa huwa mwisho wa jambo lake ni kupungukiwa na kufilisika katika mali.” [Ibn Maajah kutoka kwa Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنه)]

 

Share