278-Aayah Na Mafunzo: Matahadharisho Ya Ribaa Na Adhabu Zake

 

Al-Baqarah

Matahadharisho Ya Ribaa Na Adhabu Zake

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٢٧٨﴾

278. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa nyinyi ni Waumini

 

 

 

Mafunzo:

 

‘Awn bin Abi Juhayf amehadithia kutoka kwa baba yake kuwa alinunua kijana (mtumwa) anayejua kuumika (hijaamah). Akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza (kuchukua) thamani ya damu (malipo yatokanayo na kuumika), na thamani ya mbwa, na chumo la malaya na amemlaani mla ribaa na muwakilishi wake na mtu anayechora (ngozi za watu kwa kutia rangi ndani yake na mchorajwi na mchonga vinyago.” [Al-Bukhaariy]

 

 “Dirhamu ya ribaa anayokula mtu na huku anajua ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara thelathini na sita.” [Ahmad]

 

“Ribaa ina milango 73 iliyo nyepesi na sahali ni mtu kumuoa mamake.” [Al-Haakim]

 

“Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza… kula ribaa.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share