128-Aayah Na Mafunzo: Tukio La Uhud Kuumizwa Nabiy Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi wa Sallaam

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Tukio La Uhud Kuumizwa Nabiy Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi wa Sallaam

 

   

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

128. Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.

 

 

Mafunzo:

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka hii Kama alivyohadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoinua kichwa chake kutoka rukuu’ ya Swalaah ya Alfajir: “Allahumma Rabbanaa Lakal-Hamdu fil-Aakhirah. Kisha akasema: “Allaahumma mlaani fulani na fulani.” Ikateremka: Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.”(3: 128) [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo].

 

Na Anas bin Maalik  (رضي الله عنه)amehadithia kwamba: Siku ya Uhud, jino la Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lilivunjika na akachomwa mkuki begani mwake. Damu ikawa inamchirizika usoni mwake akawa anaifuta damu huku akisema: “Vipi watu watafaulu ikiwa wamerowanisha uso wa Nabiy wao kwa damu na hali yeye anawalingaia kwa Allaah?” Hapo ikateremka Aayah hii: Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.” (3: 128) [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh].

Share