133-Aayah Na Mafunzo: Unapoomba Jannah Omba Jannatul-Firdaws

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Unapoomba Jannah Omba Jannatul-Firdaws

 

 

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٣٣﴾ 

133. Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Rabb wenu na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa.

 

Mafunzo:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mnapomuomba Allaah Al-Jannah basi muombeni Al-Firdaws kwani hiyo ni ya juu kabisa, na ni nzuri zaidi, kutoka humo mnabubujika mito ya Jannah na sakafuni mwake iko ‘Arsh ya Ar-Rahmaan.” [Al-Bukhaariy].

 

Share