Aayah Na Mafunzo
Al-Maaidah
Tahadharisho La Kuazimia Kuua Au Kuuana
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾
27. Na wasomee (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) khabari za wana wawili wa Aadam; kwa haki walipotoa qurbaan (dhabihu) ikakubaliwa ya mmoja wao, na haikukubaliwa ya mwengine; (asiyekubaliwa) akasema: “Bila shaka nitakuua.” (Aliyekubaliwa) Akasema: “Hakika Allaah Anatakabalia wenye taqwa.”
Mafunzo:
Tahadharisho la kuazimia kuua au kuuana: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Waislamu wawili watakapokabiliana kwa panga zao, basi wote wawili; muuaji na aliyeuliwa wataingia motoni.” [Al-Bukhaariy na Muslim].