030-Aayah Na Mafunzo: Anayeua Kwa Dhulma Atabeba Dhambi Za Mwana Wa Kwanza Wa Aadam

Aayah Na Mafunzo

Al-Maaidah

Anayeua Kwa Dhulma Atabeba Dhambi Za Mwana Wa Kwanza Wa Aadam

 

 

فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٣٠﴾

 30. Basi (aliyekataliwa dhabihu,) nafsi yake ikamwezesha kwa wepesi kumuua ndugu yake; akamuua na akawa miongoni mwa waliokhasirika.

 

Mafunzo:

 

‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Haiuliwi nafsi yeyote ile kwa dhulma ila mwana wa kwanza wa Aadam atabeba pia dhambi za kumwaga damu, kwani yeye ndiye wa kwanza kutenda kitendo cha uuaji.” [Ahmad na wengineo].

 

 

Share