06-Al-Lajnah Ad-Daimah: Ameamka Na Huku Anasinzia Kisha Akanywa Maji Lakini Hakumbuki Wakati

Ameamka Na Huku Anasinzia Kisha Akanywa Maji Lakini Hakumbuki Wakati

 

Al-Lajnah Ad-Daimah

 

www.alhidaaya,com

 

 

SWALI:

 

Nimeamka usiku mmoja wa Ramadhwaan nikanywa maji yaliyoko karibu na kitanda changu, kisha nikarudi kulala. Nilipoamka nimeona watu wanarudi kutoka kuswali Alfajiri na asubuhi ilishaingia nje kweupe kabisa. Kwa hali hii nikajiuliza wakati gani nilikunywa maji? Ilikuwa kabla ya Alfajiri au baada ya Alfajiri? Najua kuwa nilikuwa nimesinzia lakini nina hakika kuwa nilikunywa maji. Je, Sheikh inanipasa niilipe siku hii au hainipasi kuilipa?

 

 

JIBU:

 

Kama hali ilikuwa kama ulivyoelezea basi iliyo sahihi ni udhanie kuwa ilikuwa ni usiku kwa hiyo funga ilikuwa ni sawa mpaka ikuthibitikie  kuwa kumbe kunywa maji huko kulikuwa baada ya kuingia  Alfajiri hapo tena itakubidi uilipe siku hiyo.

 

Allaah Atujaalie At-Tawfiyq.  Swalah na Salaam ziwe juu ya Nabiy wetu Muhammad, familia yake, na Maswahaba zake. 

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa - Fatwa Namba 4181]

 

 

Share