Uzushi Wa Du’aa Ya Mara Moja Katika Umri (Maisha)

 

Uzushi Wa Du’aa Ya Mara Moja Katika Umri (Maisha)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Tunaomba ufafanuzi kuhusu du’aa hii ambayo inaenezwa sana katika mitandao na groups mbalimbali za simu.

 

DUA YA MARA MOJA KWENYE UMRI WA BINADAMU

Amesema Mtume MOHAMAD S.A.W kwa Madhumuni Ya Hadithi Inavyosema: ATAKAYE SOMA DUA HII MDA WOWOTE

>>NI KAMA MTU ALIYOENDA HAJI MARA 360

>>NI KAMA MTU ALIYOKHITIMU QUR-AN MARA 360

>>AMEJIKOMBOA NA IBADA 360

>>NA NISAWA KAMA AMETOA SADAKA 360 DINARI

>>NA KAFARIJI 360 HUZUNI KUBWA

~Na kama Alivoyosema  Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W

Kwenye Hadithi ALISHUKA JEBREIL AKASEMA : ewe mtume wa mwenyezi mungu MJA YOYOTE KWENYE WAJA WA UMMA YAKO ATAKESOMA DUA HII HATA KAMA MARA MOJA KWENYE UMRI WA MAISHA YAKE Kwakukanusha Jalali na kuhakikisha mambo yake saba

>>ATONDOLEWA UMASKINI

>>ATAONDOLEWA SUALI LA UOVU NA NAKEER

>>ATAMURURISHWA (atapitishwa)KATIKA NJIA YAKE

>>ATAHIFADHISHWA (ataondolewa)KWENYE KIFO CHA MSHITUKO

>>ATAEPUSHWA NA MOTO

>>ATAEPUSHWA NA UBANO WA KABURI

>>ATAEPUSHWA KATIKA GHADHABU ZA SULTAN ALJAIR NA DHALIMU

(NA HII NDIO DUA)

LAILAH ILA ALLAH ALJALEEL ALJABAAR

LAILAH ILA ALLAH ALWAHED ALQAHAR

LAILAH ILA ALLAH ALKAREEM ALSTAAR

LAILAH ILA ALLAH ALKABEER ALMUUTAAAL

LAILAH ILA ALLAH WAHDA LA SHAREEKAH LAHU

ILAHA WAHED

RABAA WA SHAHED

AHADAA WA SWAMADAA

WA NAHNU LAHU MUSLIMUUN

LAILAH ILA ALLAH WAHDAHU LA SHAREEKA LAHU

ALIHA WAHEDA

RABAA WA SHAHEEDA

AHADAA WA SWAMADAA

WA NAHNU LAHU ABIDUUN

LAILAH ILA ALLAH WAHDAHU LA SHAREEKA LAHU

ALIHA WAHEDA

RABAA WA SHAHEEDA

AHADAA WA SWAMADAA

WA NAHNU LAHU QAAANITOON

LAILAH ILA WAHDAHU LA SHAREEKA LAHU

ALEHA WAHEDA

RABAA WA SHAHEEDA

AHADAA WA SWAMADAA

WA NAHNU LAHU SWABIRUUN

LAILAH ILA ALLAH MUHAMAD RASUL ALLAH

ALLAHUMA ILAYEK FAWADHTU AMRI

WA ALEYKA TAWAKALT YA ARHAMA ALRAHMEEN

 

Tusaidiane kuipitisha hata tusiwakoseshe dua hii ndugu zetu wengine

 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Haya ni maradhi yaliyotoka kwa Mashia na Masufi waliyoambukizwa baadhi ya Waislamu wasiojishughulisha na elimu, na wao wakadhani ni katika dini na kuna ujira ndani yake, wakajibidiisha kueneza du'aa za kutungwa na kusingiziwa nazo Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Du'aa nyingi kama hizi za kutungwa na kunasibishwa nazo kwa uongo na dhulma kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zinapatikana katika vitabu vya du'aa za uzushi kama "Du'aa Al-Mustajaab", "Al-Jawshan Al-Kabiyr", Du'aa ya "Kanzul-'Arsh" na vinginevyo.

 

Kamati ya Kudumu ya Utoaji Fatwa na Tafiti za Kielimu ya Saudia chini ya Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) wamesema:

"Kitabu "Ad-Du'aa Al-Mustajaab" si cha kutegemewa kwa sababu kimekusanya idadi kubwa ya Ahaadiyth dhaifu na za kutungwa.

 

[Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah, mj. 2, uk.449]

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni kitabu ambacho hakiwezi kutegemewa na mtunzi wa kitabu hicho si Mwanachuoni.

Hivyo, tumetoa tanbihi kwa muda mrefu na tumeeleza kuwa hicho kitabu si cha kutegemewa. Wasomaji wanapaswa kutanabahishwa kwamba hakitegemewi kwa sababu kimekusanya Hadiyth dhaifu na za kutungwa.

 

[Fataawa Ibn Baaz, mj. 26, uk. 354-355]

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:

“Kuna kitabu ambacho kimeenezwa sana kwa watu leo hii, na kinapatikana katika maduka ya vitabu, kinaitwa “Ad-Du’aa Al-Mustajaab” cha Muhammad ‘Abdil-Jawwaad. Ni kitabu chenye hekaya kilichokusanya du’aa za kuzushwa za Kisufi na Adhkaar ambazo zimenukuliwa bila dalili zozote kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

 

Jina la kitabu chenyewe lina maelezo ya elimu ya ghayb ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala).  Mwandishi kakiita kitabu “Ad-Du’aa Al-Mustajaab (Du’aa Zenye Kujibiwa)”, je, ni nani kamjulisha huyo mwandishi  kuwa du’aa hizo zinajibiwa? Ushahidi gani anao kwa hilo, zaidi tu ya kutaka kuwavutia watu ‘awwaam (wa kawaida wasio na elimu) na kuwahadaa kwa kitabu cha uzushi.

 

Nawashauri wasomaji (watafute na kuvitumia) vitabu vya du’aa na adhkaar vya kuaminika vilivyoandikwa na Wanachuoni weledi wenye kuaminika wa Ahlus-Sunnah:

 

1. Al-Waabil Asw-Swayyib cha Imaam Ibn Al-Qayyim

2. Al-Kalim Atw-Twayyib cha Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah

3. Al-Adhkaar cha Imaam An-Nawawiy

Vitabu hivi, havina ndani yake adhkaar za uzushi; zimekusanya adhkaar zilizopokelewa kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

Vinatosheleza na vinakidhi haja na hakuna haja ya vitabu vya masimulizi ya ngano vilivyoandikwa na wafanya mzaha, na himidi zote ni za Allaah.

 

[Majmuw’ Fataawa Fadhwiylat Ash-Shaykh Swaalih bin Fawzaan, mj. 2, uk. 697]

 

Bonyeza viungo upate maelezo zaidi kuhusu vitabu vinginveyo vya bid'ah.

 

 

 

Du’aa Ya Kanzul-'Arsh (Ganjul-'Arsh) Ni Uzushi Wa Mashia Na Masufi

 

Du'aa Za Kanzul-Arsh Na Du'aa Za Masiku Ya Wiki Zimethibiti?

 

Du’aa Ya ‘Al-Jawshan Al-Kabiyr’ (Diraya Kubwa) الجوشن الكبير

 

 

 

 

Na Allaah ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share