Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry

Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry

 

 

Vipimo 

 

Unga kikombe 1 ½

Siagi ½ kikombe

Sukari ½ kikombe

Yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jam ya peach na raspberry

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Wash oven moto wa takriban 180 – 190 Deg F
  2. Piga siagi na sukari katika mashine mpaka iwe laini na nyororo (creamy) kisha weka yai na vanilla.
  3. Tia unga kidogo kidogo uchanganye kwa mwiko wa mbao (wooden spoon).
  4. Pakaza mkononi unga uchukue vidonge ubonyeze kufanya vishimo vya kuwekea jam.
  5. Panga katika treya uliyopakaza siagi.
  6. Tia nusu yake jam ya peach na nusu jam ya raspberry
  7. Bake katika oven kiasi robo saa mpaka ziwive na kugeuka rangi ya brown light.
  8. Epua vikiwa tayari

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share