06-Ruqyah Dhidi Ya Sihri, Mashaytwaan, Majini Na Kila Aina Ya Uovu

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqyah Sihri Mashaytwaan Majini Na Kila Aina Ya Uovu.

 

www.alhidaaya.com

 

Kujikinga au kujitibu na sihri (uchawi), kuvamiwa na mashaytwaan, majini na maovu yoyote yale ni kudumisha kuisoma Qur-aan kwa ujumla. Vile vile Suwrah na Aayah zilizothibiti kuwa zinafaa ruqyah, kama Suwratul-Faatihah, Suwratul-Baqarah, Aayatul-Kursiy, Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah, Suwratul-Ikhlaasw na Al-Mu’awwidhataan  (Al-Falaq na An-Naas), Suwratul-Kaafiruwn. Vile vile ni muhimu mno kudumisha nyiradi za asubuhi na jioni ambazo zina du’aa tele za kumkinga mtu anapozisoma na baadhi yake ni zifuatazo kama zilivyothibiti katika Hadiyth:

 

((مَنْ قالَ إذا أصْبَحَ : لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير كانَ لَهُ عَدْل رَقَبَة مِنْ وَلَدِ إسْماعِيل، وَكُتِبَ لَهُ عَشر حَسَناتِ وَحُطَّ عَنْهُ عَشر سَيِّئات، وَرُفِعَ لَهُ عَشر دَرَجات وَكانَ فَي حِرْزِ مِنَ الشَّيْطانِ حَتَّى يُمْسِي، وَإنْ قَالَها إذا أَمْسى كَانَ لَهُ مِثْل ذلِكَ حَتَّى يُصْبِحُ))

((Atakayesema atakapoamka:

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

”Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr”  

 

((Hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah  Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na Himdi ni Zake na Yeye juu ya kila kitu ni Mweza ...

Itakuwa ni kama kuacha huru mtumwa katika wana wa Ismaa’iyl, na ataandikiwa mema kumi, na atafutiwa makosa kumi, atapandishwa daraja kumi, na atakuwa katika kinga ya shaytwaan mpaka afike jioni na akisema jioni atapata kama hivyo mpaka afike asubuhi)).  [Hadiyth ya Abu ‘Ayyaash (Radhwiya Allaahu ’anhu) ameisahihisha Al-Albaaniy - Swahiyh Al-Jaami’ (6418) Swahiyh Abiy Daawuwd (5077), Swahiyh Ibn Maajah (3132)]

Pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:  ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ‏.‏ فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ ‏.‏ كَانَتْ لَهُ عَدْلَ عَشْرِ رِقَابٍ وَكُتِبَتْ لَهُ مِائَةُ حَسَنَةٍ وَمُحِيَتْ عَنْهُ مِائَةُ سَيِّئَةٍ وَكَانَتْ لَهُ حِرْزًا مِنَ الشَّيْطَانِ يَوْمَهُ ذَلِكَ حَتَّى يُمْسِيَ وَلَمْ يَأْتِ أَحَدٌ أَفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ إِلاَّ أَحَدٌ عَمِلَ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ...))  

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ’anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Atakayesoma  kwa siku mara mia,

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

”Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr”

 

Basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa makosa mia moja, na atakuwa na kinga ya Shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) [Al-Bukhaariy  pamoja na Al-Fat-h, (4/95) [3293], Muslim (4/2071) [2691].

Pia kuomba:

رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ ﴿٩٧﴾

 “Rabb wangu! Najikinga Kwako kutokana na udokezi wa mashaytwaan,”

وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ ﴿٩٨﴾

 “Na najikinga Kwako Rabb wasinihudhurie.”  [Al-Muuminuwn: 97-98]

Na,

أَعـوذُ بِكَلِـماتِ اللّهِ التّـامّاتِ مِنْ شَـرِّ ما خَلَـق

A’uwdhu Bikalimati-LLaahit-ttaammati min sharii maa Khalaq

 

Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari alichokiumba  [Hadiyth ya Khawlah bint Haakim kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((مَنْ نَزلَ مَنزِلاً ثُمَّ قال: أَعُوذُ بِكَلِمات اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ، لَمْ يضرَّه شَيْءٌ حتَّى يرْتَحِل مِنْ منزِلِهِ ذلكَ))

((Atakayeteremka katika kituo (au makazi) kisha akasema: 'Auwdhu bikalimati-LLaahit-taammati min sharri maa Khalaq' - Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari Alichokiumba - hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka katika kituo (au makazi) hicho)) [Muslim (4/2080) [2708].

 

Pia kusema ifuatavyo mara tatu asubuhi na jioni ambayo imo pia katika Adhkaar za asubuhi na jioni:

بِسـمِ اللهِ الذي لا يَضُـرُّ مَعَ اسمِـهِ شَيءٌ في الأرْضِ وَلا في السّمـاءِ وَهـوَ السّمـيعُ العَلـيم (ثلاثاً)

BismiLLaahiLLadhiy laa yadhwuru ma’a-Smihi shay-un fil-ardhwi walaa fissamaai wa Huwas-Samiy’ul ‘Aliym (mara 3)

 

Kwa jina la Allaah Ambaye hakidhuru kwa jina Lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, Naye ni Mwenye Kusikia yote daima Mjuzi wa yote daima.  [Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Afaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema:

((مَنْ قَالَها ثَلاثًا إذا أصْبَحَ وَثَلاثًا إذا أمْسَى لَمْ يَضُرُّهُ شَيْء))

((Atakayesema mara tatu asubuhi na jioni hatodhuriwa na chochote)) [Abu Daawuwd (4/323) [5089, 5088]. At-Tirmidhiy (5/465) [3388], Ibn Maajah [3869], Ahmad (1/72), Taz Swahiyh Ibn Maajah (2/332), Swahiyh Abi Daawuwd (5088), Swahiyh Al-Jaami’ (5745), Majmuw’ Fataawa ibn Baaz (8/108) na Isnaad yake imepewa daraja ya Hasan na Al-‘Allaamah Ibn Baaz katika Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 39)]

Pia kuomba unapopata mafazaiko ya shaytwaan usiku:

 

 أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ وَشَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ يَحْضُرُونِ

A’uwdhu bikalimati-LLaahit-ttaammati min ghadhwabihi wa-‘iqaabihi, wa sharri ‘ibaadihi, wa min hamazaatish-shayaatwiyni wa an-yahdhwuruwni

 

((Najikinga na maneno ya Allaah, yaliotimia kutokana na ghadhabu Zake na adhabu Yake na shari ya waja Wake na vioja vya mashaytwaan na kunijia kwao))

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Basi hawatomdhuru)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy - Swahiyh Abi Daawuwd (3893), Swahiyh At-Tirmidhiy (3/171) Adhkaar ya kondosha wasiwasi usingizini au kusikia uoga na mfadhaiko]

Na unapohisi vitimbi vya mashaytwaan usome:

 

  أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ الَّتِي لاَ يُجَاوِزُهُنَّ بَرٌّ ولاَ فَاجِرٌ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ وَبَرَأَ وَذَرَأَ وَمِنْ شَرِّ مَا يَنْزِلُ مِنْ السَّمَاءِ وَمِنْ شَرِّ مَا يَعْرُجُ فِيهَا وَمِنْ شَرِّ مَا ذَرَأَ فِي الأَرْضِ وَمِنْ شَرِّ مَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمِنْ شَرِّ فِتَنِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمِنْ شَرِّ كُلِّ طَارِقٍ إلاَّ طَارِقًا يَطْرُقُ بِخَيْرٍ يَا رَحْمَنُ

A’uwdhu bikalimati-LLaahil-Ladhiy laa yujaawizuhunna barrun walaa faajirun min sharri maa khalaqa, wa baraa, wa dharaa, wa min sharri maa yanzilu minas-samaai, wa min sharri maa ya’ruju fiyhaa, wa min sharri maa dharaa fil-ardhwi, wa min sharri maa yakhruju minhaa, wa min sharri fitanil-layli wan-nnahaari wa min sharri kulli twaariqin illaa twaariqan yatwruqu bikhayri Yaa Rahmaan

 

((Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyokamilika ambayo hayapiti mwema wala muovu, na shari ya Alichokiumba, na Akakitengeneza na Akasambaza.  Na shari ya kinachoteremka kutoka mbinguni na shari ya kinachopanda huko, na shari ya kinachosambaa ardhini na shari ya inayotoka ndani yake na shari ya fitnah za usiku na za mchana na shari ya kila anayegonga usiku ila anayegonga kwa kheri Ee Rahmaan)) [Ahmad kwa Isnaad Swahiyh]

 

Itaendelea kutajwa Ruqya nyenginezo kujikinga na maovu hayo katika milango inayofutia.

 

 

 

Share