07-Ruqya: Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Kila Aina Ya Shari

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Kila Aina Ya Shari

 

www.alhidaaya.com

 

 

Zimethibiti katika Qur-aan na Sunnah du’aa tele za kujikinga na shari na dhidi ya maadui, mojawapo ni du'aa ifuatayo ya Sunnah ambayo ni mukhtasari wa kinga za aina zote za shari:

 

اللَّهُمَّ إِني أسْأَلُكَ مِنْ الْخَيْرِ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أعْلَمْ، وَأعُوذُ بِكَ مِن الشَّرِّ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ ‏‏ أعْلَمْ،  اللَّهُمَّ إِنِّي أسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَألَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا استعَاذَ  بِكَ مَنْهُ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَمَا قَرَّبَ إلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ وَأعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ، وَأسْأَلُكَ أنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا

Allaahumma inniy as-aluka minal-khayri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi, maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Wa a’uwdhu Bika min sharri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Allaahumma inniy as-aluka min khayri maa saalaka ‘Abduka wa Nabiyyuka, wa a’uwdhu Bika min sharri masta’aadha Bika minhu ‘Abduka wa Nabiyyuka. Allaahumma inniy as-alukal-Jannata wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa a’uwdhu Bika minan-nnaari wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa as-aluka antaj-’ala kulla qadhwaai qadhwaytahu liy khayraa

 

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba khayr zote zilizo karibu na mbali nizijuazo na nisizozijua. Najikinga Kwako na shari zote za karibu na za mbali nizijuazo na nisizozijua. Ee Allaah, hakika nakuomba khayr alizokuomba mja Wako na Nabiy Wako, na najikinga Kwako shari alizojikinga nazo mja Wako na Nabiy wako. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba Jannah na yanayokaribisha kwayo katika kauli au 'amali, na najikinga Kwako Moto na yanayokaribisha kwayo katika kauli au 'amali, na nakuomba Ujaalie kila majaaliwa yangu [uliyonikidhia] yawe khayr.

[Ibn Maajah – Ametaja katika mlango aliosimulia Hadiyth kwa anuani ya ‘Du’aa za  ‘Jawaami’il-Kalimi’]

 

Du’aa nyinginezo:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَمِلْتُ وَمِنْ شَرِّ مَا لَمْ أَعْمَلْ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min sharri maa ‘amiltu wamin sharri maa lam a’-amal

 

 

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari niliyotenda na shari nisiyoitenda  [Muslim, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy,  Ibn Maajah na Ahmad]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ التَّرَدِّي ، وَالْهَدْمِ ، وَالْغَرَقِ ، وَالْحَرَقِ ،  وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ يَتَخَبَّطَنِي الشَّيْطَانُ عِنْدَ الْمَوْتِ ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ فِي سَبِيلِكَ مُدْبِرًا ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ لَدِيغًا

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minat-taraddiy, wal-hadmi, wal-gharaqi, wal-haraqi, wa a’uwdhu bika an yatakhabbatwniyash-shaytwaanu ‘indal-mawti, wa a’uwdhu bika an amuwta fiy sabiylika mudbiraa, wa a’uwdhu bika an amuwta ladiyghaa

 

Ee Allaah, hakika  mimi najikinga Kwako kuangamia na kubomoka na kufa kwa kuzama na kuungua na Moto, na najikinga Kwako kughilibiwa na shaytwaan wakati wa mauti, na najikinga Kwako kufa nikiwa mwenye kugeuka nyuma katika njia Yako [kukimbia vita] na najikinga Kwako kufa kwa kung'atwa au kudungwa [na mdudu au mnyama wa sumu]. [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy  - Swahiyh An-Nasaaiy (3/1123)]

 

Pia katika nyiradi miongoni mwa nyiradi za asubuhi kama alivyohadithia Abuu Ad-Dardaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم

Hasbiya-Allaahu laa ilaaha illaa Huwa ‘Alayhi tawakkaltu wa Huwa Rabbul ’Arshil ‘Adhwiym (mara 7 asubuhi na jioni)

 

Ananitosheleza Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake Yeye nimetawakali na Yeye ni Rabb wa ‘Arsh Adhimu.

 

((من قالها حين يصبح وحين يمسي سبع مرات كفاه الله ما أهمه من أمر الدنيا والآخرة))

((Atakayesema asubuhi na jioni itamtosheleza katika mambo yake yanayomtia hamu ya dunia na Aakhirah)). [Fataawa Ibn Baaz, (9/294) Ibn As-Sunniy [71] Marfuw’ na Abuu Daawuwd Mawquwf (4/321), na isnadi yake ameisahihisha Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir Al-Arnaauwtw. Taz. Zaad Al-Ma’aad (2/376)]

 

Na du’aa ifuatayo kama ilivyotajwa katika Hadiyth na ambayo pia ni miongoni mwa nyiradi za asubuhi na jioni:

عن ابن عمر رضي الله عنهما، قَالَ: لَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يدع هؤلاء الكلمات إذا أصبح وَإذا أَمْسَى:

 

((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِينِي وَدُنْيَايَ وَأَهْلِي وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ وَمِنْ خَلْفِي وَعَنْ يَمِينِي وَعَنْ شِمَالِي وَمِنْ فَوْقِي وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ مِنْ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتـي)) صحيح: أخرجه البخاري في ((الأدب المفرد)) (1200)، وأبو داود (5074)

 

Imepokelewa kutoka kwa ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haachi kuomba mambo manne anapoamka asubuhi na jioni:

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ وَأهْـلي وَمالـي، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي، وَمِن فَوْقـي، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي

 

Allaahumma inniy as-alukal ‘aafiyah fid-dunyaa wal Aakhirah. Allaahumma inni as-alukal ‘afwa wal ‘aafiyata fiy Diyniy wa dunyaaya, wa ahliy, wa maaliy. Allaahumma-stur ‘awraatiy, wa-aamin raw’aatiy. Allaahumma-hfadhwniy min bayni yadayya, wamin khalfiy, wa ‘an yamiyniy, wa ‘an shimaaliy, wamin fawqiy, wa a’uwdhu bi’adhwmatika an ughtaala min tahtiy

 

Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al-'Aafiyah (hifadhi, amani, salama) duniani na Aakhirah. Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al-'Aafiyah katika Dini na dunia yangu, na ahli wangu, na mali yangu. Ee Allaah nisitiri aibu zangu na nitulize khofu yangu. Ee Allaah, nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, na juu yangu, na najikinga kwa Uadhimu Wako kwa kutekwa chini yangu. [Swahiyh Al-Bukhaariy katika Adab Al-Mufrad (1200), Abuu Daawuwd [5074], Ibn Maajah [3871]. Taz. Swahiyh ibn Maajah (2/332), Taz. Swahiyh Abiy Daawuwd [5074]  

 

Na kifupi yake unaweza kuomba:

  اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالأَخِرَةِ

Allaahumma inniy as-alukal-‘aafiyata fid-dunyaaa wal-Aakhirah

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba al’-aafiyah (hifadhi, amani, salama) duniani na Aakhirah   [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/180, 185, 170)]

 

Na miongoni mwa Adhkaar za asubuhi pia ni zifuatazo:

 

أَصْبَـحْـنا وَأَصْبَـحْ المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذا الـيَوْم، فَـتْحَهُ، وَنَصْـرَهُ، وَنـورَهُ وَبَـرَكَتَـهُ، وَهُـداهُ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَه.

Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaahi Rabbil ‘Aalamiyn. Allaahumma inniy as-aluka khayra haadhal-yawmi fat-hahu, wanaswarahu, wanuwrahu, wabarakatahu, wahudaahu, wa a’uwdhu Bika min sharri maa fiyhi washarri maa ba’-dahu

 

Tumeingia asubuhi  na imefika asubuhi na Ufalme ni wa Allaah Rabb wa walimwengu, Ee Allaah, hakika mimi nakuomba khayr ya siku hii ya leo, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najikinga Kwako kutokana na shari ya kilicho ndani ya siku hii, na shari ya baada ya siku hii. [Hadiyth ya Abuu Maalik Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ’anhu) ameikusanya Abuu Daawuwd (4/322) [5084], na isnadi yake ni Hasan kutoka kwa Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir Al-Arnaauwtw katika Tahqiyq Zaad Al-Ma’aad (2/273)].

 

Jioni useme:

 

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذهِ اللَّـيْلَة، فَتْحَهـا، وَنَصْـرَهـا، وَنـورَهـا، وَبَـرَكَتَـهـا، وَهُـداهـا، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهـاِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَهـا.

 

Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah Rabbil ‘Aalamiyn. Allaahumma inniy as-aluka khayra haadhihil-laylati fat-hahaa, wanaswarahaa, wanuwrahaa, wabarakatahaa, wahudaahaa, wa a’uwudhu Bika min sharri maa fiyhaa washarri maa ba’dahaa

 

Tumeingia jioni na imefika jioni na Ufalme ni wa Allaah, Rabb wa walimwengu, Ee Allaah hakika mimi nakuomba khayr ya usiku huu, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najikinga kwako kutokana na shari ya kilicho ndani ya usiku huu, na shari ya baada ya usiku huu.

 

Pia:

 

أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هَذا الْيَوْمِ  وَخَـيرَ ما بَعْـدَهُ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هَذا الْيَوْمِ  وَشَرِّ ما بَعْـدَهُ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر  

 

Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaah wal-HamduliLlaah. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhal yawmi wakhayra maa ba’-daahu, wa a’uwdhu bika minsharri haadhal yawmi washarri maa ba’-dahuu, Rabbi a’uwdhu bika minal kasali wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin fil qabri

 

Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah, na Himdi ni Zake Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah, hali yakuwa Peke Yake, Hana mshirika. Ni Wake Ufalme, na Himdi ni Zake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Rabb wangu, nakuomba khayr ya siku ya leo, na khayr ya baada ya siku hii, na ninajikinga Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na uvivu, na ubaya wa uzee ubaya. Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas‘wud (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - Muslim (4/2088) [2723]

 

 

Na ikiingia jioni useme:

 

 أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر

 

Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah wal-HamduliLLaahi. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhihil-laylati wakhayra maa ba’dahaa, wa a’uwdhu bika minsharri haadhihil-laylati washarri maa ba’dahaa, Rabbi a’uwdhu bika minalkasli wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin filqabri

 

 

Nyinginezo ni du’aa ifuatayo ambayo ni miongoni mwa du’aa za usiku wakati wa kulala:

 

اللَّهُمَّ رَبَّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الأَرْضِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، رَبَّنَا وَرَبَّ كُلِّ شَيْءٍ، فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوَى، وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ وَالْفُرْقَانِ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شَيْءٍ أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الآَخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَيْءٌ ، اقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْر

 

Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-‘i wa Rabbal-ardhwi, wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, Rabbanaa wa Rabba kulli shay-in, faaliqal-habbi wan-nnawaa, wa munzilat-Tawraati wal-Injiyli  wal-Furqaan. A’uwdhu bika min sharri kulli shay-in Anta aakhidhun binaaswiyatihi. Allaahumma Antal-Awwalu falaysa qablaka shay-un, wa Antal-Aakhiru falaysa ba’-daka shay-un wa Antadhw-Dhwaahiru falaysa fawqaka shay-un, wa Antal-Baatwinu falaysa duwnaka shay-un. Iqdhwi ‘annad-dayna wagh-ninaa minal-faqri  

 

Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba na Rabb wa ardhi, na Rabb wa ‘Arsh ‘Adhimu, Rabb wetu na Rabb wa kila kitu, Mpasuaji wa mbegu na kokwa na Aliyeiteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Najikinga Kwako shari ya kila kitu, Wewe Ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah, Wewe Ndiye Al-Awwalu (wa Awali hakuna kitu kabla Yako) na Al-Aakhiru (wa Mwisho hakuna kitu baada Yako) na Adhw-Dhwaahiru (Uliye juu hakuna kitu juu Yako), na Al-Baatwinu (Uliye karibu, hakuna kitu kilicho karibu kuliko Wewe), Nilipie madeni yangu na Niepushe na ufakiri.  [Muslim]

 

Tanbihi:

 

Tumezitaja humo baadhi ya adhkaar za asubuhi, jioni na usiku lakini hizo si zote, kwa hiyo nasaha ya dhati na muhimu kabisa ni kwamba Muislamu asiache kabisa kudumisha Nyiradi za asubuhi na jioni ambazo zimekusanya baadhi ya Suwrah na Aayah na du’aa mbali mbali za kumhifadhi dhidi ya kila aina ya maovu yakiwa ni shirki au shari za mashaytwaan na majini, au viumbe viovu na kila lenye shari.

Hali kadhaalika, kunapatikana kudumisha kuisoma Qur-aan na yaliyothibiti yote kama yalivyotangulia kutajwa.

 

 

 

 

Share