08-Ruqyah: Kuomba Kinga Kwa Allaah Kutokana Na Jirani Muovu

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kuomba Kinga Kwa Allaah Kutokana Na Jirani Muovu

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Unapokuwa na jirani muovu huwa ni mtihani kwa sababu ya kukosa amani kutokana na shari zake. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba kinga dhidi ya jirani muovu na ameamrisha tujikinge naye:

  

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنْ جَارِ السَّوْءِ فِي دَارِ الْمُقَامِ فَإِنَّ جَارَ الْبَادِيَةِ يَتَحَوَّلُ عَنْكَ))  رواه النسائي (5517) وأبو يعلى (6536) وابن حبان (1033) والحاكم (1951)

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ombeni kinga kwa Allaah kutokana na jirani muovu katika sehemu za makazi ya kudumu kwani jirani wa jangwani hubadilika badilika kuhama)) [An-Nasaaiy, Abuu Ya’laa (6536), Ibn Maajah (1033), Al-Haakim (1951) na ameisahihisha Imaam  Al-Albaaniy - Swahiyh An Nasaaiy (5517), As-Silsilatusw-Swahiyhah (3943),   Swahiyh Al-Jaami’ (2967)]

Ufafanuzi: Makazi ya kudumu: Makazi ya kuthibitika hayabadiliki; watu hubakia hawaondoki kuhama kuhama.

 

Hivyo basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba:

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السَّوْءِ فِي دَارِ الْمُقَامِ فَإِنَّ جَارَ الْبَادِيَةِ يَتَحَوَّلُ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min jaaris-saw-i fiy daaril-muqaami fainna jaaral-baadiyati yatahawwalu.

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na jirani muovu katika makazi ya kudumu kwani jirani wa jangwani hubadilika badilika kuhama)) [As-Silsilat Asw-Swahiyhah (3943), Swahiyh Al-Jaami’ (2967)]

 

Pia alikuwa akiomba:

أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ  يَوْمِ السُّوءِ وَمِنْ لَيْلَةِ السُّوءِ وَمِنْ سَاعَةِ السُّوءِ وَمِنْ صَاحِبِ السُّوءِ وَمِنْ جَارِ السُّوءِ  فَي دَارِ الْمُقَامَةِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min yawmis-suw-i wamin laylatis-suw-I, wamin saa’atis-suw-i, wamin swaahibis-suw-i, wamin-jaaris suw-i fiy daaril-muqaamat

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako kutokana na siku ovu, na usiku muovu, na saa ovu, na rafiki muovu, na jirani muovu katika makazi ya kudumu. [Atw-Twabaraaniy katika  Majma’ Az-Zawaaid (10/144), Swahiyh Al-Jaami’ (1/411)]

 

Pia:

 اللَّهُمَّ إنِّي أّعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السُّوءِ، وَمِنْ زَوْجٍ تُشَيِّبُنِي قَبْلَ المَشِيبِ، وَمِنْ وَلَدٍ يَكُونُ عَليَّ رَبّاً، وَمِنْ مَالٍ يَكُونُ عَلَيَّ عَذَابَاً، وَمِنْ خَلِيْلٍ مَاكِرٍ عَيْنُهُ تَرَانِي، وَقَلْبُهُ يَرْعَانِي؛ إِنْ رَأَى حَسَنَةً دَفَنَهَا، وَإِذَا رَأَى سَيِّئَةً أَذَاعَهَا 

 الطبراني في الدعاء، 3/ 1425، برقم 1339، وهناد في الزهد، برقم 1038، وقال الألباني في سلسلة الأحاديث الصحيحة، 7/ 377، برقم 3137 :  قلت: وهذا إسناد جيد، رجاله كلهم من رجال التهذيب

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min jaaris-suw-i, wa min zawjin tushayyibuniy qablal-mashiybi, wa min waladin yakuwnu ‘alayya rabban, wamin maalin yakuwnu ‘alayya ‘adhaaban, wamin khaliylin ‘aynuhuu taraaniy wa qalbuhu yar’aaniy, in raa hasanah dafanahaa, wa idhaa raa sayyiah adhaa’ahaa

Ee Allaah, najikinga Kwako kutokana na jirani muovu, na kutokana na mke atakayenisababisha uzee kabla ya uzee na kutokana mwana atakayekuwa ni bwana kwangu anayenidhibiti, na kutokana na mali itakayokuwa ni adhabu kwangu, na kutokana na rafiki mwandani khaini; ambaye macho yake yananitazama lakini huku moyo wake unaniangaza kwa hila kiasi kwamba anapoona zuri  hulificha, lakini  anapoliona baya hulitangaza. [Atw-Twabaraaniy katika Ad-Du’aa (3//1425) [1339] na Hunaad katika Az-Zuhd (1038) na Al-Albaaniy amesema katika As-Silsilat Asw-Swahiyhah (7/377) [3137]:  Nimesema hii ni Isnaad nzuri, watu wake wote ni katika watu wa kuaminika]

 

Haipasi jirani kumfanyia jirani mwenzake uovu wowote ule, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameamrisha kumfanyia wema, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa. [An-Nisaa: 36]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ ،  وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ ،  وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ!))  قِيلَ: مَنْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟  قَالَ: الَّذِي لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَائقَهُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wa-Allaahi hakuamini (hana Iymaan). Wa-Allaahi hakuamini, Wallaahi hakuamini!)) Akaulizwa: Nani ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

وَفِي رِوَايَة: ((لاَ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مَنْ لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَائِقَهُ)) مسلم

Na katika riwaaya nyengine: ((Hatoingia Peponi ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake)).[Muslim]

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا زَالَ جِبْرِيلُ يُوصِينِي بِالْجَارِ حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ)). متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jibriyl hakuacha kuniusia jirani mpaka nikadhani kuwa atawafanya warithi wangu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

 

Share