Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Kuua Vidudu Vyenye Madhara Nyumbani Kama: Mende, Mbu, Nzi...

 

Hukmu Ya Kuua Vidudu Vyenye Madhara Nyumbani Kama: Mende, Mbu, Nzi... 

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, inajuzu kuua vidudu vinavyopatikana nyumbani kama sisimizi, mende na aina hizo? Na je, kuwaua kuwe kwa maji au kuwaunguza? Na kama haijuzu tufanyeje?

 

 

JIBU:

 

Wadudu hao ikiwa wanaleta maudhi inajuzu kuwaua kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

Viumbe watano vinafaa kuuliwa; ikiwa mtu yuko katika hali ya ihraam au hali yenye kuruhusiwa;  nao ni kunguru, mwewe, panya, nge na mbwa kichaa.

 

Na katika Hadiyth nyingine imetaja nyoka.

 

Lakini si kuwaunguza moto.

 

Na hii Hadiyth sahihi inajulisha kuwa inajuzu kuua vilivyotajwa, na katika vile vyenye maana kama hivyo vyenye kuleta maudhi au madhara kama vile mbu, nzi, mende, sisimizi, wanyama pori, mdugu chungu. Lakini ikiwa sisimizi haleti madhara haifai kuwaua kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuua sisimizi na nyuki na hud-hud (ndege)  na kipanga (ndege). Vikiwa havileti maudhi yoyote  (basi havitakiwi kuuliwa).

Ama ikipatikana kutoka kwake (sisimizi) madhara, basi ataingia kwenye lile fungu (juu) lililotajwa kwenye hiyo Hadiyth.

 

Na Tawfiyq ni kutoka kwa Allaah.

 

 

 

 

Share