Mambo Gani Ya Kumfanyia Mtoto Anapozaliwa?

Mambo Gani Ya Kumfanyia Mtoto Anapozaliwa?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam aleykum warahmatullah wabarakatuh. Naombeni anayejuwa dua, unapojifungua siku hiyo na mtt apewe nini kabla hajanyonya? mimi sijui nasikia kuna dua rasmi na kuna kitu anapewa mtt kwa ajili ya kinga za dunia.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Wa 'Alaykumus Salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuhu

 

Wanachuoni wanaeleza kuwa hakuna du'aa maalum iliyopokelewa kuhusu mtoto anapozaliwa.

Isipokuwa wanasema kuwa mtu akipenda anaweza kumuombea mtoto du'aa yoyote njema za salama, makuzi mema na uongofu.

 

 

Yaliyothibiti kufanyiwa mtoto baada ya kuzaliwa

 

 

Kumfanyia Tahniyk

 

Jambo lililothibiti kufanyiwa mtoto anapozaliwa ni kupendezwa kufanyiwa tahniyk na kumuombea du'aa.

 

Tahniyk ni kumlambisha mtoto kitu kitamu kama kuitafuna tende ilainike na kumlambisha au hata asali.

 

 

Amesimulia Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu):

"Nilipata mtoto wa kiume, nikampeleka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akampa jina la Ibraahiym na akamfanyia tahniyk kwa baadhi ya tende na kumuombea baraka na kunirejeshea."

[Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Kumpa Mtoto Jina Siku Ya Kwanza Au Ya Saba

 

Kadhaalika, inafaa kumpa jina mtoto siku ya kwanza au siku ya saba wakati anapofanyiwa 'Aqiyqah.

'Aqiyqah ni kumchinjia siku ya saba baada ya kuzaliwa, mtoto wa kiume kondoo au mbuzi wawili, na ikiwa ni mtoto wa kike anachinjiwa kondoo au mbuzi mmoja.

 

Tumeona hapo juu ushahidi wa kumpa mtoto jina siku ya kwanza anapozaliwa, na vilevile ushahidi mwengine ni huu:

 

Inasimuliwa kuwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Alizaliwa mtoto kwangu wa kiume usiku huu na nikampa jina la baba yangu Ibraahiym (Nabiy Ibraahiym 'Alayhis-Salaam)."

[Muslim]

 

Imesimuliwa kuwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwafanyia 'Aqiyqah Al-Hasan na Al-Husayn katika siku ya saba, na akawapa majina."

[Al-Haakim, Ibn Hibbaan, na Ibn Hajar kasema ni sahihi katika Fat-hu Al-Baariy, mj. 9, uk. 589]

 

 

Kumfanyia Mtoto 'Aqiyqah Na Kumtahiri

 

Maelezo kuhusu 'Aqiyqah ni marefu na yanapatikana hapa kwenye kiungo chini:

 

'Aqiyqah Anayofanyiwa Mtoto Mchanga Katika Sunnah

 

 

Kutahiri

 

014-Swahiyh Fiqhis-Sunnah: Kutahiri

 

 

Hayo ndio mambo muhimu ya kumfanyia mtoto anapozaliwa.

 

Kuhusu majina ya kumpa mtoto, hapa chii kuna faida zaidi:

 

Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto

 

 

 

Na Allaah ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

Share