03-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Wanawake Kuharakiza Mwendo Baina Ya Nguzo Za Kijani Katika Sa’y

 

 

Wanawake Kuharakiza Mwendo Baina Ya Nguzo Za Kijani Katika Sa’y

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Katika elimu yangu ndogo niliyopata katika vitabu vya Fiqh, Milango ya Hajj na 'Umrah, sikuona kukatazwa mwanamke kuharakiza mwendo baina ya nguzo za kijani katika Sa’y. Niliwahi kumsikia Shaykh wa televisheni akisema kuwa mwanamke hakimbii eneo hilo bali ni kwa ajili ya wanaume tu. Hii ni kwa sababu ya kuhifadhika zaidi kwa wanawake kwa kutokudhihirisha yanayosababisha fitna akiwa anakimbia. Lakini hakutaja dalili yoyote katika kauli yake. Hivyo nikawaza kuwa ikiwa rai yangu ni sawa, basi kukimbia ni Sunnah aliyoianzisha Bibi Haajar (Radhwiya Allaahu 'anhaa). Hata hivyo naheshimu rai ya Shaykh, na Himdi Anastahiki Allaah kuwa Shariy’ah za  Dini yetu haziundwi tu kutokana na rai (zisizostahili) kama alivyosema Amiyrul-Muuminiyn 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu). Tafadhali naomba nasaha Allaah Akubariki, kwani mara kwa mara huenda kutekeleza 'Umrah na familia yangu, hivyo tunahitaji kujua yaliyo sahihi kuhusu mas-ala haya.

 

 

JIBU:

 

Ibn Al-Mundhir kasema:

"’Ulamaa wamekubaliana kwamba mwanamke asikimbie katika eneo la Nyumba (Ka'bah) au eneo la Sa’y (Swafaa na Marwa) baina ya nguzo za kijani. Hii ni kwa sababu kufanya hivyo ni kuonyesha ushupavu na nguvu, jambo ambalo halikukusidiwa kwa wanawake. (Mfano pia kuweka ridaa (sehemu ya juu ya nguo ya ihraam) kwapani. Mwanamke anatakiwa kujifunika asitirike, na kwa vile kukimbia kunahitaji kuweka ridaa (kuvaa rubega), itasababisha kumdhihirisha sehemu ya mwili wake."

 

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 226, Swali Namba 5 la Fatwa Namba 8820 -   Imejumuisha:

 

Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz Ibn 'Abdillaah bin Baaz

 

Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy

 

Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah bin Ghudayyaan

 

Mjumbe: Shaykh 'Abdullah bin Qu'uwd]

 

 

Share