07-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kukata Nywele Pembeni Tu Mwa Kichwa

 

Kukata Nywele Pembeni Tu Mwa Kichwa

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Tunaona baadhi ya watu katika Hajj wanakata nywele pembezoni tu mwa vichwa vyao wakiacha sehemu nyingine yote ya kichwa bila ya kuguswa. Tulipowafahamisha kuwa  nywele zinatakiwa zikatwe sawa sawa kichwa kizima, walikanusha na kudai walivyofanya ni sawa. Je, ni sawa hivyo?

 

JIBU:

 

Wajibu ni kunyoa nywele zote, au kukata sawasawa kote kichwani, katika fardhi ya Hajj au 'Umrah. Haimpasi mtu kukata sehemu fulani tu ya kichwa. Hivyo ilivyotajwa katika Swali sio sawa kama zilivyo rai sahihi za ‘Ulamaa na wala sio Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 217, Swali Namba 5 la Fatwa Namba 1734 -   Imejumuisha:

 

Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdul-’Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz

 

Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy 

 

Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Qu’uwd]

 

 

Share