Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

 

Vipimo

 

Unga -  4 Vikombe vya chai

Siagi - 1 Kikombe cha chai

Hiliki   ½ Kijiko cha chai

 

Shira: 

Sukari - 2 Vikombe vya chai

Maji   - 1 Kikombe cha chai

Vanilla  ½ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
  2. Changanya vizuri isiwe na madonge.
  3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
  4. Halafu utakata sampuli  unayopenda mwenyewe.
  5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto  usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
  6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
  7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
  8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai.
  9. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya  nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share