07-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Suluhu

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَلصُّلْحِ

07-Mlango wa Suluhu[1]

 

 

 

735.

عَنْ عَمْرِو بْنِ عَوْفٍ اَلْمُزَنِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {اَلصُّلْحُ جَائِزٌ بَيْنَ اَلْمُسْلِمِينَ، إِلَّا صُلْحاً حَرَّمَ حَلَالاً وَ أَحَلَّ حَرَاماً، وَالْمُسْلِمُونَ عَلَى شُرُوطِهِمْ، إِلَّا شَرْطاً حَرَّمَ حَلَالاً وَ أَحَلَّ حَرَاماً} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ

 وَأَنْكَرُوا عَلَيْهِ. لِأَنَّ رَاوِيَهُ كَثِيرَ بْنَ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوِ بْنِ عَوْفٍ ضَعِيفٌ.  وَكَأَنَّهُ اِعْتَبَرَهُ بِكَثْرَةِ طُرُقِهِ

   وَقَدْ صَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ

 Kutoka kwa ‘Amr bin ‘Awf Al-Muzaniyy[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Suluhu[3] inafaa baina ya Waislamu isipokuwa suluhu inayoharamisha halaal[4] au inayohalalisha haraam.[5] Waislamu wako juu ya masharti yao isipokuwa sharti inayoharamisha halaal au inayohalalisha haraam.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]

Ulamaa wameikataa Hadiyth hii kwa sababu mpokezi wake ni Kathiyr bin ‘Abdillaah bin ‘Amr bin ‘Awf ni dhaifu.[6]

Ibn Hibbaan ameisahihisha kutoka katika Hadiyth iliyopokewa na Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

 

 

 

736.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {لَا يَمْنَعُ جَارٌ جَارَهُ أَنْ يَغْرِزَ خَشَبَةً فِي جِدَارِهِ. ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ مَا لِي أَرَاكُمْ عَنْهَا مُعْرِضِينَ؟ وَاَللَّهِ لَأَرْمِيَنَّ بِهَا بَيْنَ أَكْتَافِكُمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jirani asimkataze jirani yake kusimamisha mbao katika ukuta wake.”[7] Kisha Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa akisema: “Mbona nawaona mumeiacha Sunnah hii? Wa-Allaahi mtaibeba baina ya mabega yenu (hata mkichukia)” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

737.

وَعَنْ أَبِي حُمَيْدٍ اَلسَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {لَا يَحِلُّ لِامْرِئٍ أَنْ يَأْخُذَ عَصَا أَخِيهِ بِغَيْرِ طِيبِ نَفْسٍ مِنْهُ} رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ فِي "صَحِيحَيْهِمَا" 

Kutoka kwa Abuu Humayd As-Saa’idiyy[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si halaal kwa mtu kuchukua fimbo ya nduguye bila ya nafsi yake kuridhia.”[9] [Imetolewa na Ibn Hibbaan na Al-Haakim katika Swahiyh zao]

 

 

[1] Suluhu ni kuweka muafaka baina ya watesi wawili, kama vile mtu kudai haki ya mwengine kwa kuamini kuwa yeye ndiye mwenye haki kuliko mwingine.

 

[2] Huyu ni ‘Abdullaah ‘Amr bin ‘Awf bin Zayd bin Milha Al-Muzaniyy (kutoka katika kabila la Muzaynah), ni babu wa Kathiyr bin ‘Abdillaah. Alisilimu mapema, alihuduria Badr na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa mamlaka ya kusimamia Msikiti wa Madiynah. Alikuwa ni mwenye taqwa na mwenye kububujikwa na machozi katika ‘Ibaadah. Ni Swahaba, alifariki katika utawala wa Mu’aawiyah.

 

[3] Katika lugha ya kiarabu Sulhu ina maana ya amani. Kuna aina nyingi za suluhu kama vile suluhu baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu, suluhu baina ya mke na mume, suluhu baina ya serikali na waasi, magomvi ya kibiashara na suluhu za mambo ya fedha. Katika Hadiyth hii inakusudiwa aina hii ya mwisho ya suluhu. Migogoro ya kifedha ina mikataba ambayo ni halaal na kuna isiyokuwa halaal na masharti ya mikataba yenyewe.

 

[4] Msingi wa mwanzo muhimu wa mkataba ni kuwa isiwe kinyume na shariy’ah na isibadilishe haraam kuwa halaal na halaal kuwa haraam. Kama vile kusuluhisha juu ya kuchukua mali isiyo halali kwake.

 

[5] Kama vile kumtaka mume asilale kwa mke wa pili.

 

[6] Ash-Shaafi na Abuu Daawuwd wamemtaja kuwa ni “Msingi wa uongo”. Ahmad amesema: “Hadiyth zake ni Munkar.” An-Nasaaiy naye amemzungumzia kwa kusema: “Haaminiki” na Ibn Hibbaan amesema: “Ana kitabu cha Hadiyth alichokitunga akisingizia kuwa amepokea kutoka kwa baba yake nae kutoka kwa babu yake.”

 

[7] Shariy’ah imejali maingiliano ya kijamii na kuiwekea miongozo kama hili la jirani kuweka mbao kuegemea ukuta wa jirani yake.

 

[8] Huyu ni Abuu Humayd As-Saa’idiyy. Jina lake ni Al-Mundhir bin Sa’d. alihudhuria vita vya Uhud na vilivyofuatia baada yake, aliishi hadi mwaka wa 60 Hijriyyah.

 

[9] Hadiyth hii ni dalili kuwa ni haraam kuchukua mali ya Muislamu hata ikiwa ni kidogo kiasi gani ila kwa radhi yake.

Share