08-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Mlango Wa Hawala Na Dhamana

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ الْحَوَالَةِ وَالضَّمَانِ

08-Mlango Wa Hawala[1]Na Dhamana[2]

 

 

 

738.

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَطْلُ اَلْغَنِيِّ ظُلْمٌ، وَإِذَا أُتْبِعُ أَحَدُكُمْ عَلَى مَلِيٍّ فَلْيَتْبَعْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَفِي رِوَايَةِ أَحْمَدَ: {فَلْيَحْتَلْ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kuchelewesha tajiri (kulipa deni) ni dhulma. Na mmoja wenu atakapofuatishwa kwa mwenye uwezo na afuate.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

739.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {تُوُفِّيَ رَجُلٌ مِنَّا، فَغَسَّلْنَاهُ، وَحَنَّطْنَاهُ، وَكَفَّنَّاهُ، ثُمَّ أَتَيْنَا بِهِ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَقُلْنَا: تُصَلِّي عَلَيْهِ ؟ فَخَطَا خُطًى، ثُمَّ قَالَ: " أَعَلَيْهِ دَيْنٌ ؟ " قُلْنَا: دِينَارَانِ، فَانْصَرَفَ، فَتَحَمَّلَهُمَا أَبُو قَتَادَةَ، فَأَتَيْنَاهُ، فَقَالَ أَبُو قَتَادَةَ: اَلدِّينَارَانِ عَلَيَّ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  "أُحِقَّ اَلْغَرِيمُ وَبَرِئَ مِنْهُمَا اَلْمَيِّتُ؟ " قَالَ: نَعَمْ، فَصَلَّى عَلَيْهِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ

 Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Alikufa mtu miongoni mwetu, tukamuosha, tukamtia dawa na tukamkafini, kisha tukamuendea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) tukamuambia: Utamswalia? Akaenda hatua chache akasema: Ana deni? Tukasema: Ana deni la dinari mbili. Akaondoka. Abuu Qataadah akabeba deni lile (akalidhamini) tukamuendea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Qataadah akamuambia: zile dinari mbili juu yangu. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Haki ya mdai (kulipwa) na je maiti ameepukana nayo? Akasema ndio. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamswalia.”[3] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]

 

 

 

740.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  كَانَ يُؤْتَى بِالرَّجُلِ اَلْمُتَوَفَّى عَلَيْهِ اَلدَّيْنُ، فَيَسْأَلُ: "هَلْ تَرَكَ لِدَيْنِهِ مِنْ قَضَاءٍ ؟ " فَإِنْ حُدِّثَ أَنَّهُ تَرَكَ وَفَاءً صَلَّى عَلَيْهِ، وَإِلَّا قَالَ: "صَلُّوا عَلَى صَاحِبِكُمْ " فَلَمَّا فَتَحَ اَللَّهُ عَلَيْهِ اَلْفُتُوحَ قَالَ: " أَنَا أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ، فَمَنْ تُوُفِّيَ، وَعَلَيْهِ دَيْنٌ فَعَلَيَّ قَضَاؤُهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ:{فَمَنْ مَاتَ وَلَمْ يَتْرُكْ وَفَاءً}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa analetewa mtu aliyekufa anayedaiwa Anauliza: Ameacha cha kulipa deni lake? Akiambiwa kuwa ameacha[4] humswalia, la si hivyo alikuwa akisema Mswalieni Swahibu yenu. Allaah alipomfungulia alikuwa akisema: Mimi ni aula kwa Waumini kuliko nafsi zao, atakayekufa ilhali anadaiwa basi ni juu yangu kulipa deni lake.”[5] [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah ya Bukhaariy: “Atakayekufa na hakuacha cha kulipia deni lake…”

 

 

 

741.

وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا كَفَالَةَ فِي حَدٍّ} رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ 

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna udhamini katika hadd (adhabu).”[6] [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

[1] Hawala ina maana mbili: Ya kwanza ni mtu kumhakikishia tajiri kuwa deni lake litarudi. Hii inaruhusiwa kishariy’ah. Ya pili ni kuhamisha deni kutoka katika dhima ya mmoja hadi kwa mwingine.

 

[2] Dhamana ni kujitwika deni la mwenye kudaiwa.

 

[3] Ina maana kuwa deni au haki yoyote ya mwanadamu, haitosamehewa mpaka lilipwe au lisamehewe na mhusika. Hata baada ya kifo chake deni bado linasimama pale pale. Kadhalika tunajifunza katika Hadiyth hii mtu kumdhamini deni la maiti hata kama si jamaa yake.

 

[4] Yaani ameacha mali ya kutosha.

 

[5] Ni juu yangu kulilipa haikuwa na maana mali yake binafsi Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Wakati huo hazina ya dola ilikuwa chini ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ndio maana akasema: “Ni juu yangu kumlipia.” Jukumu hili lilikuja kuhamia kwa mkuu wa nchi kama Hadiyth nyingine itakayokuja kufafanua. Hadiyth hii imefuta Hadiyth iliyotangulia. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa hana uwezo alikuwa hamswalii maiti anayedaiwa kwa sababu Swalaah yake ni Shafaa (maombezi) inayokubaliwa moja kwa moja. Lakini alipopata uwezo jukumu la madeni lilikuwa juu yake. Na katika utawala wa Kiislamu kiongozi anawajibika kumlipia maiti deni lake, asipofanya hivyo dhambi ni zake.

 

[6] Huduwd: adhabu iliyowekwa na Shariy’ah katika Uislam. Hakuna dhamana katika huduwd. Kwa mfano, hakutakiwi kuwepo na dhamana kwa wizi, uzinzi, kumkashifu mtu na ulevi. Kuna sababu nyingi kwa nini hairuhusiwi dhamana kwa makosa haya:
i. kimsingi dhamana hutumika kutilia nguvu ushahidi, wakati katika utekelezaji wa huduwd, jambo la msingi ni kuwepo kwa ushahidi dhidi ya mtuhumiwa inadhoofishwa na mashtaka yaende kwa mtuhumiwa.

ii. Dhamana huchelewesha maamuzi, na hakuna hakika kuwa mtuhumiwa atathibitika katika utuhumiwa wake na ataadhibiwa. Ikiwa tuhuma itathibitika, hivyo basi hakuna haja ya maombi ya msamaha wa huduwd.

iii. Mdhamini anatakiwa amlete mdhaminiwa kwenye hukumu mahakamani; kutokuwepo kwa mtuhumiwa majukumu yake atabebeshwa mdhamini. Hata hivyo adhabu za huduwd zinatekelezwa kwa mhalifu na sio kwa mtu mwingine yeyote. Hadiyth hii ingawa Isnaad yake ni dhaifu lakini maana yake ni sahihi kwa ‘Ulamaa. Iwapo kutakuwepo na udhamini katika adhabu anayopewa mtu bila shaka shariy’ah za adhabu zitabatilika.

Share