34-Zawadi Kwa Wanandoa: Kulidekeza Jina La Mke

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

34-Kulidekeza Jina La Mke

 

ترخيم اسم الزّوجة 

 

 

Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alimuita 'Aaishah jina lake kwa kulidekeza na kumuita 'Aaishu. Na lengo la mwito huu ni kuonesha mapenzi kwa mke na kujikurubisha nae.

 

Hivyo basi ni juu ya waume kujifunza kutoka kwa kiongozi wetu pindi wanapocheza na wake zao, kwani katika haya ni raha tupu kwa yule atakaemudu kuifanya vizuri fani hii aliyotufundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Na katika dekezo la namna hii ni kuonesha mapenzi ya kweli na inapelekea katika ladha na kusisimsha shauku na kuwafurahisha wote pamoja.

 

Share