44-Zawadi Kwa Wanandoa: Asimgongee Mwanamme Kumgongea Mke Wake Usiku

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

44-Asimgongee Mwanamme Kumgongea Mke Wake Usiku

 

 ألاّ يطرق الرجل أهله لي

 

 

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik:

 

 أنّ النبي صلى الله عليه وسلم كان لا يطرق أهله ليلا كان يدخل غدوة أو عشاء

“Kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alikuwa hagongi kwa mkewe usiku, alikuwa akiingia asubuhi sana au ishaa.” (Al-Bukhaariy na Ahmad)

 

Kutoka kwa ibn Umar (Radhiya Allahu 'anhuma) anasema kuwa:

وعن ابن عمر أنّ رسول الله صلى الله عليه وسلم نزل العقيق فنهى عن طروق النساء , فعصاه رجلان , فكلاهما رأى ما يكره.

“Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alishukia alghaqiiq akakataza kugongewa wanawake, watu wawili wakamuasi (wakenda kugonga kwao) na wote wawili waliona mambo yaliyowachukiza.” (Ahmad)

 

Hali kadhalika kutoka kwa 'Abdullaah bin Rawaaha kwamba siku moja alikuwa amerudi kutoka safari akachelewa, na akaona nyumbani kwake pana waka taa, na mke wake anacho kitu pamoja nae, akaamua kuchukua upanga, akasema mkewe: koma usinisogelee, ni mwanamke Fulani ananisuka, akajiwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  katika hilo na akakataza wanaume kuwagongea milango wake zao usiku.(Ahmad)

Share