015-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Adhaana

Hiswnul-Muslim

015-Du’aa Za Adhaana

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

[22]

 

Mtu akisikia Muadhini anaadhini anatakiwa asema kama anavyosema Muadhini, ila atakapo sema:

حَـيَّ عَلـى الصَّلاة

 

Hayya ’alasw-Swalaah

 

Njooni kwenye Swalaah

 

 حَـيَّ عَلـى الْفَـلاح

 

Hayya ’alal falaah

 

Njoni kwenye mafanikio

 

Yeye hatomuigiza bali anatakiwa aseme:

لا حَـوْلَ وَلا قُـوَّةَ إِلاّ بِالله

 

Laa Hawla walaa quwwata Illaa biLLaah[1]

 

Hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah.

 

 

[23]

 

Muadhini akisema:

أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ اللهُ أَشْـهَدُ انَّ مُحَمدا رَسُول الله

 

 Ash-hadu anlaa Ilaaha illa Allaah, ash-hadu anna Muhammada Rasuwlu Allaah.

 

Anatakiwa mtu aseme:

 

وَأَنا أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ اللهُ وَحْـدَهُ لا شَـريكَ لَـه وَأَنَّ محَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه رَضيـتُ بِاللهِ رَبَّاً، وَبِمُحَمَّـدٍ رَسـولاً،  وَبِالإِسْلامِ دينَـاً .

Wa anaa ash-hadu an laa ilaaha illaAllaah Wahdau laa shariyka Lah, wa anna Muhammadan ’Abduhu wa Rasuwluhu, Radhwiytu biLLaahi Rabban wabi Muhammadin Rasuwlan wabil Islaami Diynaa.

Na mimi pia nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Mmoja Peke Yake, Hana mshirika na kwamba Muhammad ni mja Wake, na Rasuli Wake. Nimeridhika kuwa Allaah Ndiye  Rabb wangu, na kuwa Muhammad ni Rasuli wangu, na kuwa Uislamu ndio Dini yangu[2].

 

Sema hivyo baada ya tashahhad ya Muadhini[3]

 

 

 [24] 

 

Kisha baada ya kumjibu Muadhini mswalie Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وسلم)[4]  

Kisha sema:

 

اللّهُـمَّ رَبَّ هَذِهِ الدّعْـوَةِ التّـامَّة وَالصّلاةِ القَـائِمَة آتِ محَـمَّداً الوَسيـلةَ وَالْفَضـيلَة وَابْعَـثْه مَقـامـاً مَحْـمُوداً الَّذي وَعَـدْتَه [5]

Allaahumma Rabba haadhihidda’watit ttaammah, wasw-swalaatil qaaimah, aati Muhammadanil wasiylata walfadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdani lladhiy wa’adtah. (Innaka laa Tukhliful-Miy’aad.. Haikuthibiti)

 

Ee Rabb wa wito huu uliotimu, na Swalaah ya kudumu! Mpe Muhammad Wasiylah na daraja ya juu zaidi, na Mfufue Umpe Maqaam ya kuhimidiwa Uliyomwahidi[6]

 

[26]

 

Ajiombee mtu baina ya Adhaana na Iqaamah kwani du’aa wakati huo hairudishwi[7]

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (1/125), Muslim (1/288)

 

[2]Hadiyth ya Sa’ad bin Abi Waqqaasw (رضي الله عنه)  Muslim (1/290)

 

[3]Ibn Khuzaymah (1/220)

 

[4]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akisema:

 

إذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوامِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا . ثُمَّ سلُوا اللَّه لي الْوسِيلَةَ ، فَإِنَّهَا مَنزِلَةٌ في الجنَّةِ لا تَنْبَغِي إِلاَّ لعَبْدٍ منْ عِباد اللَّه وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُو ، فَمنْ سَأَل ليَ الْوسِيلَة حَلَّتْ لَهُ الشَّفاعَةُ

 

((Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi, na kisha niombeeni (kupata) ‘wasiylah’ ambayo ni manzila (heshima maalum) huko Jannah. Haitomstahikia isipokua mja mmoja katika waja wa Allaah, nami ninatarajia kuwa mja huyo, na mwenye kuniombea “wasiylah” atapata uombezi (wangu Siku ya Qiyaamah)) - Muslim (1/288)

 

[5] Tanbihi: Kauli ya ziyada ni Dhwa’iyf:

انك لا تخلف الميعاد

Innaka Laa Tukhliful-Miy’aad 

 

‘Ulamaa wamesema kuwa haikuthibiti kama alivyorekodi Imaam Al-Albaaniy katika As-Silsilah Adhwa’iyfah [6714]

 

[6]Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما)  - Al-Bukhaariy, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

((مَنْ قالها حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ))

((Mwenye kusema hivo, atapata uombezi wangu siku ya Qiyaamah))

 

 

[7]Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه)  - At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, Ahmad na taz Irwaa Al-Ghaliyl  (1/262)

 

 

 

 

Share