Mkate Wa Ufuta

Mkate Wa Ufuta

      

Vipimo:   (vya kutokea mikate  6)

Unga- 3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Tui la nazi au maziwa  - 2 ½ (Mugs)

Hamira - 1 Kijiko cha supu

Chumvi - Kiasi

Sukari - 1 kijiko cha chai

Yai - 1

Ufuta - Kiasi

Mafuta au samli Ya kupakia mkate - Kiasi

  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Changanya pamoja unga, nazi, chumvi, hamira, sukari na yai.  Hakikisha unga wote umetoka madonge na umevurugika vizuri uwe laini. (uwe maji maji kama wa kaimati lakini unakuwa mzito kidogo kuliko wa kaimati).
  2. Usubiri uumuke (Ufure)

Jinsi Ya Kuchoma Mikate:

  1. Hakikisha chuma cha kuchomea kiwe kinagandisha vizuri (Kisiwe non- stick) na pia kisiwe kilichopikiwa mafuta.
  2. Weka chuma  kwenye moto, kikipata moto rushia maji ya chumvi kidogo halafu tia unga  kiasi kama kiganja kimoja cha mkono, utawanye vizuri kwa vidole halafu nyunyizia  ufuta juu yake.
  3. Ukianza kuwa mkavu nyanyua chuma   kifudikize  kwenye moto mpaka mkate wako uwe rangi ya dhahabu.
  4. Toa kwenye chuma kwa kutumia kisu.
  5. Paka samli au mafuta juu ya mkate  kwa tumia brush.
  6. Endelea hivyo hivyo mpaka umalizie unga wote.

 

Share