17-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Swahaba Walikatazwa Kumwita Kama Wanavyoitana Wao Kwa Wao Au Kwa Jina Lake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

17-Swahaba Walikatazwa Kumwita Kama Wanavyoitana Wao Kwa Wao Au Kwa Jina Lake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَّا تَجْعَلُوا دُعَاءَ الرَّسُولِ بَيْنَكُمْ كَدُعَاءِ بَعْضِكُم بَعْضًا ۚ قَدْ يَعْلَمُ اللَّـهُ الَّذِينَ يَتَسَلَّلُونَ مِنكُمْ لِوَاذًا ۚ فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾

Msifanye wito wa Rasuli baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Kwa yakini Allaah Anawajua miongoni mwenu wale wanaoondoka kwa kunyemelea. Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo. [An-Nuwr: 63]

 

Adhw-Dhwahaak amesema kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) kwamba amesema: “Walikuwa wakisema: “Yaa Muhammad, Yaa Abal-Qaasim” basi Allaah Akawakataza hivyo kwa sababu ya kumtukuza Nabiy Wake, baada ya hapo wakawa wanasema: “Yaa Nabiyya-Allaah, Yaa Rasuwla-Allaah.” Mujaahid na Sa’iyd bin Jubayr (Rahimahumaa-Allaah) nao pia wamsema hivyo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

Imaam As-Sa’dy (Rahimahu-Allaah) naye amesema kuhusu kusudio la Aayah hiyo kwamba: Msiseme: “Yaa Muhammad bin ‘Abdillaah” Kama mnavyoitana wenyewe kwa wenyewe bali (Allaah) Amemtukuza na Akamfadhilisha na Akamtofautisha na wengineo wamwite: “Yaa Rasuwla-Allaah, Yaa Nabiyya-Allaah.”

 

 

Share