18-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Alipojulisha Khabari Zake Alimtaja Kwa Sifa Tukufu Kabisa

  Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

18-Allaah Alipotaka Kujulisha Khabari Zake Alizijulisha Bila Kumtaja Jina,

Isipokuwa Alimtaja Kwa Sifa Tukufu Ya ‘Ubuwdiyyah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah ('Azza wa Jalla) Alipotaka kujulisha khabari za Nabiy Wake, Alizijulisha bila ya kumtaja kwa jina lake kwa ajili ya kumtukuza Nabiy Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamtaja kwa kumpa sifa tukufu nayo ni sifa ya Al-‘Ubuwdiyyah[1] (kumwabudu Allaah kikamilifu).  Basi Allaah ('Azza wa Jalla) Akamtaja kwa sifa hiyo katika Aayah kadhaa za Qur-aan; miongoni mwanzo ni pale Alipomuelezea katika safari ya Al-Israa wal-Mi’raaj; Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١﴾

Utakasifu ni wa Ambaye Amemsafirisha usiku mja Wake kutoka Al-Masjid Al-Haraam mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake; ili Tumuonyeshe baadhi ya Aayaat (miujiza, ishara, dalili) Zetu. Hakika Yeye (Allaah) ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Al-Israa: 1]

 

Na Akasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu safari hiyo hiyo ya Al-Israa Wal-Mi’raaj:

 

فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ ﴿١٠﴾

(Allaah) Akamfunulia Wahy mja Wake yale Aliyomfunulia Wahy. [An-Najm: 10]

 

Na katika hali ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumwabudu na kumuomba du’aa Rabb wake:

 

وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا﴿١٩﴾

Na kwamba mja wa Allaah (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) aliposimama kumwomba (Rabb wake), walikaribia kumzonga. [Al-Jinn: 19]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجًا ۜ﴿١﴾

AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Ambaye Amemteremshia mja Wake (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu na wala Hakukifanya ndani yake kiwe kombo. [Al-Kahf: 1]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

هُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٩﴾

Yeye Ndiye Yule Anayemteremshia mja Wake Aayaat bayana ili Akutoeni katika viza na kukuingizeni kwenye Nuru. Na hakika Allaah kwenu ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [Al-Hadiyd: 9]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. [Al-Baqarah: 23]

 

 

 

[1] Maana Ya Al-‘Ubuwdiyyah kwa upana kidogo: Unyenyekevu, mapenzi, khofu ya adhabu za Allaah na kutaraji rahma za Allaah, utiifu na udhalili kwa Allaah Aliyetukuka, na kutovuka mipaka Yake, na kutekeleza maamrisho Yake na kujizuia na makatazo Yake, kwa kujikurubisha kwa Allaah na kutaka thawabu Zake na kujihadhari na ghadhabu na ikabu Zake.

 

 

 

Share